May 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ousmane Dembele

Tetesi za soka Ulaya leo Alhamisi 08.10.2020

Ousmane Dembele

Mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele 23 hakuwa na hamu ya kujiunga na Manchester United kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho na sasa anataka kujiunga na Juventus msimu ujao.(Catalunya Radio, via Mirror)

Klabu ya Manchester United haitawasilisha ombi la kumsajili mchezaji wa Senegal na Watfotd Ismaila Sarr, 22, kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho la ligi ya EFL tarehe 16. (Goal)

Danny Rose

Kocha wa Tottenham Jose Mourinho, anatarajia kumpiga chini beki wa kushoto wa England Danny Rose, mwenye umri wa miaka 30, katika kikosi chake cha wachezaji 25 ambacho kinatarajiwa kukamilika kufikia tarehe 20 Oktoba. (Mail)

Mchezaji wa Westaham raia wa Brazil, Felipe Anderson amesema anafikia ndoto yake ya kushiriki katika mechi za ligi ya klabu bingwa Ulaya, baada ya kuhamia katika klabu ya Porto kwa mkopo katika kipindi cha msimu kilichosalia , lakini anaamini kwamba bado ataendelea kuichezea West (Talksport)

West Ham ina mpango wa kuongezea beki wa kati kutoka ligi ya daraja la kwanza nchini England huku wakitafuta kiungo wa kati atakayeziba pengo lililowachwa na Anderson . (London Evening Standard)

Kipa wa Manchester United na Argentina Sergio Romero, mwenye umri wa miaka 33, anajiandaa kuhamia katika ligi ya Marekani ya MLS baada ya kukosa kujiunga na klabu ya Everton katika siku ya mwisho wa dirisha la usajili. (Mail)

Mkufunzi mpya wa Nottingham Forest Chris Hughton anafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Fulham raia wa Ufaransa Anthony Knockaert, mwenye umri wa miaka 28, kwa mkopo. (Sky Sports)

West Brom wana imani ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Huddersfield na Karlan Grant, mwenye umri wa miaka 23, kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho katika ligi ya EFL Ijumaa ijayo. (Mail)

Mkufunzi wa Ujerumani Joachim Low anadai kwamba beki wa Chelsea raia Ujerumani Antonio Rudiger alijaribu kufanya kila kitu kuondoka Chelsea kabla ya siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho na anaamini kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 atawasilisha ombi la kutaka kuondoka katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.. (Sun)

Callum Hudson Odoi

Bayern Munich, ambao walishindwa kuafikiana kuhusu mkataba wa kumsajili kwa mkopo winga wa England Callum Hudson Odoi mwenye umri wa miaka 19, waliambiwa na Chelsea kwamba watapewa adhabu iwapo mchezaji huyo hatashirikishwa katika mechi nyingi katika ligi ya Bundesliga mbali na kifungu cha sheria cha Bayern kumnunua kwa zaidi ya pauni milioni 70 iwapo atacheza idadi fulani ya mechi. (Sport Bild)

Kiungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish, mwenye umri wa miaka 25, amefichua kampeni yake ya wiki tatu ya kumshawishi kiungo wa kati wa England Ross Barkley kujiunga na klabu hiyo kutoka Chelsea. (London Evening Standard)

Grealish alikuwa mmoja wa wachezaji wanne waliokuwa wakilengwa na mkufunzi wa Man United Solskjaer ambaye alishindwa kuwasaini kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa. (ESPN)

Mshambuliaji mpya wa Manchester United na Uruguay Edinson Cavani, mwenye umri wa miaka 33, amefichua kwamba anataka kuichezea klabu ya Boca Juniors baada ya kuondoka katika uwanja wa Old Trafford.. (Goal)

%%%%%%%%%%%%%%%%