May 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dele Alli,Tottenham

Tetesi za soka Ulaya leo 21.09.2020

Na Mwandishi Wetu TimesMajira Online

Dele Ali

Kiungo wa Tottenham na timu ya Taifa ya England Dele Alli, anahusishwa na mipango ya kuhamia Paris St-Germain, hiyo imekuja baada ya kuachwa kwenye kikosi kilichoibuka na ushindi mwishoni mwa wiki dhidi ya Southampton. (Mail)

Mustakabali wa beki wa Chelsea Antonio Rudiger uko mashakani, baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichokubali kichapo mwishoni mwa iki dhidi ya Liverpool, licha ya kwamba Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 27 hana majeruhi (Mail).

Alexandre lacazette
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anasema Klabu hiyo haiko kwenye mazungumzo na Alexandre Lacazette kuhusu mkataba mpya, mshambuliaji huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 29, amebakiza miaka miwili ya mkataba kusalia kwenye klabu hiyo.

Fulham imetuma ofa ya kumnasa mlinzi wa Sassuolo Marlon, kwa mujibu wa mkurugenzi wa klabu hiyo Giovanni Carnevali, mazungumzo yanaendelea kuhusu uhamisho wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 25. (Sky Sports Italia, via Football Italia)

Alex Telles

Beki wa klabu ya Porto inayoshiriki Ligi Kuu Ureno Alex Telles, raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 27, amesisitiza kwamba lengo lake kwa sasa ni kuichezea klabu hiyo, licha ya kuhusishwa kuhamia Manchester United. (Sport TV, via Metro)

Luke Shaw

Mlinzi wa kushoto wa Manchester United na England Luke Shaw, mwenye umri wa miaka 25, amesema klabu hiyo inapaswa kufanya usajili zaidi, ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho cha Old Trafford. (TV2, via Manchester Evening News)

Crystal Palace inaongoza katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa timu ya Liverpool, Rhian Brewster mwenye umri wa miaka 20, huku vilabu vya Sheffield United na West Brom vikionyesha nia ya kumsajili nyota huyo wa timu ya vijana ya England ya chini ya miaka 21. (Mail).

Liverpool haina mpango wa kumuuza kiungo wa timu hiyo na England Alex Oxlade-Chamberlain, mwenye umri wa miaka 27, anayehusishwa na timu ya Wolves. (Mirror).

Leicester City inatarajiwa kuungana na Tottenham kutaka kumsajili beki wa Beijing Guoan na Korea Kusini Kim Min-jae, 23. (90min)

Kiungo wa zamani wa Manchester United Ravel Morrison, mwenye umri wa miaka 27, anatarajiwa kujiunga na klabu ya ADO Den Haag ya Uholanzi, baada ya kutemwa na Sheffield United. (Omroep West, via Football Oranje)

Arturo Vidal
Kiungo wa Chile Arturo Vidal, mwenye umri wa miaka 33, atafanyiwa vipimo vya afya leo hii kabla ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Barcelona kwenda Inter Milan. (Marca)