December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tetesi za soka Ulaya

Rais wa Napoli Aurelio de Laurentiis anasema mchezaji wa safu ya ulinzi Msenegal Kalidou Koulibaly, 29, ataondoka kwa bei inayofaa msimu huu, huku Manchester United na Manchester City zikiongoza katika kasi ya kusaini nae mkataba. (Talksport)

Manchester United na Manchester City zinapambana kumpata Kalidou Koulibaly

Manchester City wako tayari kwa dau jipya la pauni milioni 66 na zaidi na nyongeza kwa ajili ya Koulibaly wiki ijayo. (Inside Futbol)

Frank Lampard siye aliyekuwa na nia ya kumleta Kai Chelsea kwa mara ya kwanza
Maelezo ya picha,Frank Lampard siye aliyekuwa na nia ya kumleta Kai Chelsea kwa mara ya kwanza

Lengo la Chelsea la kumnunua kiungo wa kati wa kimataifa wa Ujerumani Kai Havertz, 21, kutoka klabu ya Bayer Leverkusen ilitokana mmliliki wa klabu hiyo Roman Abramovich na wala sio meneja Frank Lampard. (Express)

Mshambuliaji mpya wa Chelsea Mjerumani Timo Werner, 24, alikataa fursa ya kuhamia Manchester City baada ya kocha Pep Guardiola kumuita wajadili uwezekano wake wa kuhama. (Mail)

Barcelona wamekubali kanuni za kumsaini Memphis Depay
Maelezo ya picha,Barcelona wamekubali kanuni za kumsaini Memphis Depay

West Ham wameweka dao la thamani ya zaidi ya pauni milioni £20 kwa ajilili ya kiungo wa kati-nyuma Burnley Muingereza James Tarkowski, 27. (Sky Sports)

Barcelona wamekubali kanuni za kumsaini winga wa Uholanzi Memphis Depay, 26, kutoka klabu ya Lyon ya Ufaransa. (Teamtalk)

Manchester Unted wamejiandaa kuacha nia ya kumsaini Jadon Sancho
Maelezo ya picha,Manchester Unted wamejiandaa kuacha nia ya kumsaini Jadon Sancho

Meneja wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino amepinga madai yaliyotolewa awali kwamba hatawahi kuwa meneja wa Barcelona kwasababu ya kuwatii mahasimu wake Espanyol. (Sun)

Manchester United wanajiandaa kuacha jaribio lao la kusaini mkataba na winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho kwasababu wanahisi kuwa thamani ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 aliyopewa na klabu yake ya Ujerumani ni ya kiwango cha juu. (Star)

Manchester United hawatashusha thamani ya Chris Smalling
Maelezo ya picha,Manchester United hawatashusha thamani ya Chris Smalling

Manchester United pia hawako tayari kushusha thamani yao ya pauni milioni 18 waliyomthamanisha difenda Muingereza Chris Smalling, 30, lakini kuna matumaini kwamba mkataba na Roma unaweza bado kufikiwa. (Corriere Dello Sport, via Star)

Ofa ya Tottenham kwa kiungo wa kati wa Barcelona Lucas de Vega imekataliwa na upande wa La Liga . Ingawa De Vega anataka kuhama, Barca wanataka kumfaya sehemu kubwa ya timu B yao msimu ujao. (Sport – in Spanish)

Alexandre Lacazette ni miongoni mwa wachezaji ambao Arsenal imewatoa kwa ofa
Maelezo ya picha,Alexandre Lacazette ni miongoni mwa wachezaji ambao Arsenal imewatoa kwa ofa

Arsenal imewatoa kwa ofa wachezaji wawili -Ufaransa Matteo Guendouzi na Alexandre Lacazette katika mkataba wa kubadilishana wachezaji kwa ajili ya Mghana mwenye umri wa miaka 27 na kiungo wa kati wa Atletico Madrid Partey. (Mirror)

Leeds wako katika mazungumzo na Feyenoord juu ya mshambuliaji Crysencio Summerville, huku kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 “akiruhusiwa kuondoka” klabu ya Uholanzi kwa ajili ya kujiunga na Elland Road. (Leeds Live)

Barcelona wana uhakika Georginio Wijnaldum anaweza kutoka Liverpool
Maelezo ya picha,Barcelona wana uhakika Georginio Wijnaldum anaweza kutoka Liverpool

Barcelona wana uhakika kwamba kiungo wa kati Georginio Wijnaldum, 29, anaweza kushawishiwa atoke Liverpool katika kipindi hiki cha dirisha la uhamisho. (Goal)

Aston Villa imefanikiwa katka mazungumzo juu ya mkataba wa kumsaini mshambuliaji wa timu ya Brentford Ollie Watkins, 24. (Football Insider)

West Ham wamekataa gharama ya malipo aliyopangiwa Mualgeria Said Benrahma
Maelezo ya picha,West Ham wamekataa gharama ya malipo aliyopangiwa Mualgeria Said Benrahma

Aston Villa imekataliwa dau lake kwa ajili ya mshambuliaji Muingereza wa kabu ya Bournemouth Callum Wilson, mwenye umri wa miaka 28, rejected. (Talksport)

West Ham wanakataa kulipa pauni milioni 20 kwa ajili ya mshambuliaji Mualgeria Said Benrahma, 25 ambacho ndicho kiwango cha thamani yake iiyowekwa na Brentford. (Telegraph)

Juventus inaendelea kufanya kila liwezekanalo kumpata Tanguy Ndombele
Maelezo ya picha,Juventus inaendelea kufanya kila liwezekanalo kumpata Tanguy Ndombele

Tottenham wamejipanga kupewa ofa ya mchezaji mahiri wa Italia -Federico Bernardeschi, 26, kama sehemu ya juhudi za Juventus za kusaini mkataba na kiungo wa kati Mfaransa Tanguy Ndombele, 23, kutoka klabu ya kaskazini mwa London . (CalcioMercato – in Italian)

Barcelona wana nia ya kumuondoa kikosini Samuel Umtiti
Maelezo ya picha,Barcelona wana nia ya kumuondoa kikosini Samuel Umtiti

Barcelona wana nia ya kumuhamisha difenda Samuel Umtiti, 26, nje ya klabu. (Mundo Deportivo)

Sevilla ina matumaini ya kuendelea kuwa na beki wa Real Madrid Sergio Reguilon kwa mkopo kwa msimu mwingine licha ya Mhispania huyo, 23, kuhusishwa na uhamisho wa kudumu hadi Manchester United. (Marca – in Spanish)