Rais wa Napoli Aurelio de Laurentiis amesema wanataka kumsajili mlinzi wa Arsenal ,Mgiriki, 32, Sokratis Papastathopoulos, hatua ambayo inaweza kutoa mwaya kwa Kalidou Koulibaly, 29, kujiunga na Manchester City. (Standard)
De Laurentiis anakubali kwamba anajuta kutomuuza Koulibaly mapema. (Manchester Evening News)
Baba yake Lionel Messi amejadiliana na Barcelona kwa siku ya pili mfululizo juu ya uwezekano wa kijana wake kuhama klabu hiyo, na mlinzi wa Liverpool Andy Robertson anasema ni matumaini yake kwamba mshambuliaji huyo, 33, wa Argentina hatasajiliwa na timu nyingine ya ligi ya primia
Mlinzi wa Manchester United Chris Smalling, 30, anaonekana kuwa tayari kujiunga na Roma kwa mkataba wa kudumu. (Mirror)
Monaco imekataa ofa kutoka kwa Manchester United ya mlinzi wa Ufaransa, 19,
Manchester United inajaribu kumaliza suala la mshahara na kima cha uhamisho kwa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho kabla ya kutoa ofa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England. (Star)
Sevilla ina matumaini ya kuendelea kuwa na beki wa Real Madrid Sergio Reguilon kwa mkopo kwa msimu mwingine licha ya Mhispania huyo, 23, kuhusishwa na uhamisho wa kudumu hadi Manchester United. (Marca – in Spanish)
Arsenal inakaribia kukamilisha makubaliano ya mkopo ya kumsajili kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania Dani Ceballos kwa msimu wa pili kufuatana. (Mail)
Arsenal inafikiria kumtafuta kiungo wa kati wa West Ham, MBrazil Felipe,27, Anderson. (Football Insider)
Liverpool haitakubali kiungo wa kati wa Welsh Harry Wilson, 23, kuondoka tena kwa mkopo licha ya Newcastle, Leeds na Southampton kuonesha nia ya kutaka
Chelsea imearifiwa kwamba lazima ilipe pauni milioni 30 kumsajili mlinda lango wa Senegal Edouard Mendy, 28, kutoka Rennes. (Telegraph)
Inter Milan itahitajika kutafuta pesa kwa kumuuza kiungo wa kati wa Croatia Ivan Perisic ikiwa itataka kutoa ofa kwa mchezai wa Chelsea, 29, na kiungo wa kati wa Ufaransa N’Golo Kante. (Gazzetta dello Sport – in Italian)
Crystal Palace, West Ham, West Brom, Norwich na Watford zinamnyatia mlinzi wa Ufaransa, 26, Jean-Claude Billong, anayecheza katika ligi ya Serie B Salernitana. (Teamtalk)
Roma inafikiria kumchukua mshambuliaji wa Hertha Berlin na Poland Krzyszt wa Piatek kuchukua nafasi ya Edin Dzeko. (Gazzetta dello Sport – in Italian)
Hull City inatafuta kumsajili beki wa kati wa kati wa Southampton Alfie Jones, 22, kwa mkataba wa kudumu. (Yorkshire Post)
Kiungo wa kati wa Bayern Munich Mhispania Javi Martinez, 32, amedhamiria kufikia makubaliano kurejea Athletic Bilbao msimu huu. (Goal)
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM