October 12, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TEN/MET yamwaga Mil.60 kuboresha elimu Momba

Na Moses Ng’wat, Momba

Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) umetumia Sh milioni 60 kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule za msingi Wilaya ya Momba, mkoani Songwe, kwa kujenga madarasa, kutoa madawati na kugawa viti mwendo kwa watoto wenye ulemavu.

Hayo yalibainishwa, Oktoba 10, 2026, na
Mkurugenzi wa TEN/MET, Martha Makalla, wakati wa makabidhiano ya miradi na vifaa hivyo yaliyofanyika wilayani Momba, ikiwa ni sehemu y maadhimisho ya juma la elimu nchini yaliyoandaliwa na mtandao huo.

Alisema fedha hizo zimetumika katika miradi ya ujenzi kwa kurabati madarasa mawili, utoaji wa madawati 76 na viti mwendo vitatu, lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya elimu kwa watoto, wakiwemo wenye mahitaji maalum.

Makalla alisema suala la kuboresha elimu si jukumu la Serikali au taasisi moja pekee, bali kunahitaji ushirikiano wa wadau na jamii ili kila mtoto apate mazingira bora ya kujifunzia.

Akifafanua zaidi, alisema Sh milioni 23 zilitumika kujenga darasa katika Shule ya Msingi Chiwanda, huku Sh milioni 27 zikitumika kujenga darasa katika Shule ya Msingi ya Mahitaji Maalum Ndalambo.

Aidha, alisema madawati 76 yenye thamani ya Sh milioni tano yalitolewa kwa shule za msingi Msia na Ndalambo, pamoja na viti mwendo vitatu vyenye thamani ya Sh milioni mbili kwa watoto wenye ulemavu Ndalambo.

Makalla aliongeza kwa kusema TEN/MET iliamua kuunga mkono ujenzi wa darasa katika Shule ya Msingi ya Mahitaji Maalum Ndalambo baada ya kubaini juhudi za wananchi kuanzisha ujenzi huo, lakini wakashindwa kuendelea na kazi kutokana na uwezo wao kuwa mdogo.

Kwa upande wake, Chifu wa jamii ya Momba katika Kata ya Nkangamo, Chikanamulilo, alisema mchango huo unakidhi mahitaji halisi ya watoto kwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza ushiriki wao, wakiwemo wenye ulemavu.

Naye Ofisa elimu Awali na Msingi wa Wilaya ya Momba, Michael Nzunda, aliipongeza TEN/MET kwa mchango huo na kutoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono juhudi za kuboresha elimu,

Wakati, Amina Muyala, Mkazi wa Ndalambo, yeye alisema mtandao huo umesaidia kukamilisha miundombinu ambayo wananchi walishindwa kuendeleza kwa muda mr