
Na Israel Mwaisaka, Nkasi
MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya nyanda za juu kusini
kwa kushirikiana na jeshi la Polisi mkoani Rukwa wameendela Kutoa elimu kwa jamii juu ya kukabiliana na vitendo vya kihalifu mtandaoni.
Akizungumza kwenye mikutano mbalimbali inayoshirikisha wananchi wengi katika Wilaya Nkasi Leo Septemba 12,2026 meneja wa TCRA Kanda ya nyanda za juu kusini Batholomeo Titus amedai kuwa bado mkoa Rukwa una matukio mengi ya uhalifu mtandaoni kiasi cha kuiunganisha nguvu na jeshi la Polisi katika kukabiliana na vitendo hivyo.

Alisema kuwa kulingana na ripoti za utafiti mkoa Rukwa bado unashikilia nafasi ya pili kitaifa kwa vitengo vya kihalifu mtandaoni ikiongozwa na mkoa Morogoro na kudai kuwa katika mazingira hayo kunahitajika kukusanya nguvu ya pamoja miongoni mwa wadau wote katika kukabiliana na vitendo hivyo vya utapeli mtandaoni.
Titus amefafanua kuwa kinachowaumiza mamlaka ya mawasiliano Tanzania ni kuona vitendo hivyo vikiwa vikubwa kwa mkoa Rukwa ukilinganisha na miji na majiji mengine makubwa na kuwa wanatafuta chanzo kikuu cha tatizo hilo na kubwa wamejikita katika utoaji wa elimu kwani jamii ikielewa ipasavyo Kuna asilimia kubwa ya kuweza kukabiliana na changamoto hiyo.
Aliwataka Wananchi kuendelea kuchukua hatua kwa kuripoti vitendo vya uhalifu mtandaoni Polisi ikiwa ni pamoja na zile Namba za simu kuziripoti mamlaka ya mawasiliano (TCRA) na kuwa nguvu ikiwa ni pamoja Kuna uwezekano mkubwa kupungua kwa tatizo hilo.

Akitoa takwimu Mhandisi Titus alisema kuwa mkoa wa Rukwa una jumla ya matukio 1330 kwa wilaya ya Sumbawanga, Kalambo 612, na wilaya ya Nkasi matukio 553.
Kaimu kamanda wa Polisi mkoa Rukwa SSP Zacharia Bura aliwataka Wananchi kuwa makini na vitendo vya uhalifu wa mtandaoni kwani vimeleta madhara makubwa kwa jamii hasa wale waliotapeliwa kutokana na matukio ya uhalifu ya kimtandao.
Alisema vita hii ni kubwa Inahitaji mshikamano kati ya Wananchi,mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA na jeshi la Polisi kwa kuhakikisha matukio yote ya kihalifu yanaripotiwa kwa wakati na kuwa tayari Kutoa ushahidi pale inapohitajika ili kukabiliana na vitendo hivyo.




More Stories
Tuzo shindani kuongeza tija ya sekta ya Maziwa
Mwenyekiti Act Wazalendo Dodoma ahaidi siasa za hoja
Ndejembi aagiza maandalizi kukabiliana na El-nino