Na Mwandishi Wetu,Dar
MKUU wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar-es-Salaam Edward Mpogolo, ameagiza Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam kushirikiana na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini( TARURA )kuzibua mitaro na chemba zote za kupitisha maji Kariakoo wilayani humo.
 Mpogolo, ametoa agizo hilo Septemba 12,2026 wakati wa kampeni endelevu ya usafi wa kila jumamosi ilioshirikisha kampuni za usafi, KANJERE, SATEK, TIRIMA, wafanyabishara na machinga,ambapo ametaka waanze kazi ya kuzibua na kuondoa takakata katika mifereji ambazo zinasababisha maji kushindwa kupitia na kusababisha madhara wakati wa mvua.

Mpogolo amesema,Mamlaka ya Hali ya Hewa imeshatangaza uwepo wa mvua kubwa za El-nino hivyo mifereji hiyo ambayo imeziba italeta madhara wakati wa mvua hizo isipo zibuliwa.
Pia amewaagiza wakandarasi wa kampuni za kuzoa takataka wa halmashauri hiyo kuhakikisha kila njia panda wanaweka vifaa maalum vya kubeba takataka na zitakapo jaa wazipeleke dampo .
Huku akiwataka wafanyabishara wa Ilala kila mmoja kuwa na kifaa cha kuifadhia takataka kwani wao ndio wazalishaji wa taka nyingi kila siku ambazo zinasababisha mifereji ya maji kuziba.
“Tunatoa agizo kwa wafanyabishara wote wanaotupa takataka chini ya meza zao,wakikamatwa watapewa adhabu ya kufungiwa shughuli zao za biashara,”amesema Mpogolo.
Hata hivyo ameagiza barabara zote wilayani Ilala kufungwa taa kwa ajili ya usalama na kupendezesha jiji hilo ambalo linafanya biashara saa 24 kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi.Â
Sanjari na hayo ameitaka TARURA na TANROADS kuanzia sasa kutotoa vibali ovyo vya ujenzi katika barabara badala yake watafute utaratibu mwingine.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Rajabu Amiry ameaema,wasanii ni sehemu ya watu kwani usafi ni kipimo cha utu,hivyo wanaendelea warashitiki kila Jumamosi na kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan za kulipendezesha jiji hilo kwa kufanya usafi.


More Stories
TCRA, Polisi na mkakati wa kudhibiti uhalifu mtandaoni Rukwa
Tuzo shindani kuongeza tija ya sekta ya Maziwa
Mwenyekiti Act Wazalendo Dodoma ahaidi siasa za hoja