May 2, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Taulo za kike 200 zatolewa mashuleni katika matawi ya ZIC

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

KATIKA Kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia Taasisi na Makampuni wasisitizwa kuwakumbuka watoto wakike Mashuleni na kuwapa Elimu ya hedhi salama Ili kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuendelea kuzalishwa kwa viongozi mbalimbali.

Akizungumza wakati wakukabidhi Taulo za kike katika Shule ya Sekondari Ben Bella iliyopo wilaya ya Magharibi kisiwani Zanzibar Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) Salma yusuph amesema wakati wanawake wanaendelea kumsherehekea Mwanamke ni vyema kukajengeka nguzo imara kuanzia Kwa Mabinti na kuhakikishia wanakuwa kwenye Afya Bora na usalama pamoja na kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo Afya zao na kuhakikisha wanapata Hedhi Salama.

Hata hivyo ameongeza kuwa kutoa zawadi hiyo katika shule ya “Ben Bella” ni Muendelezo katika Kuiadhimisha siku hiyo ya kipekee Kwa Wanawake na wataendelea kuonyesha upendo huo katika Matawi mbalimbali nchini ikiwemo Arusha,Mtwara ,Dodoma na hata hivyo tayari wamekabidhi box kadhaa wa Kwa wanafunzi wa shule ya Pius iliyopo Kongowe jijini Dar es salaam.

“Ili awe kiongozi tunaemtaka ni lazima kufanyike jitihada za kuona Kwa jinsi gani Binti alieko shule anakuwa na Afya Bora hususani anapata Hedhi Salama na kupitia Majukumu yetu ya kibima kuhakikisha usalama wa wali ni matumaini yetu hivyo hivyo Kwa wanafunzi wetu tunawahakikisha hedhi iliyo salama kabisa.”

Aidha Kwa upande wake Afisa Biashara na uwekezaji LuLu Mohamed amewasihi wanafunzi hao kuwa na nidhamu Ili waweze kufikia na kutimiza ndoto zao na kuwataka kuendelea kusoma Kwa bidii kwani yeye ni Mmoja wa zao la shule ya “Ben Bella” na hatimae Kwa Sasa ameshika nafasi kubwa Serikalini.

“Viongozi waongoza nchi hii wengi ni Wanawake hata mimi Nina nafasi kubwa na chimbuko lake ni hapa shule ya Ben Bella nimesoma hapa na hatimae nilifauli vizuri Masoko yangu hivyo mjitahidi kusoma Kwa bidii Ili muweze kuwa alama nzuri Kwa Shuleni yenu na Taifa Kwa ujumla.”

Nae Mwalimu Msaidizi wa shule hiyo alitoa bi.Minza amepongezi za dhati Kwa uongozi wa Shirika hilo kuwapa kipaumbele wanafunzi wa shule hiyo kupatiwa taulo hizo za kujikinga wawapo katika siku zao.

”tunashukuru Kwa zawadi hizi na zimefika muda sahihi kabisa uhitaji Kwa hapa shuleni ulikua ni mkubwa Kwa Mabinti zetu hivyo kipekee tunawashukuru na tumepokea zawadi hizi .”

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Ben Bella Sekondari Bi.Mwaminza akitoa neno la shukrani Kwa uongozi wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) Kwa kuchagua shule hiyo kama sehemu ya kuwakumbuka wanafunzi hasa Mabinti na kuwapatia taulo za Kike
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ben Bella iliyopo wilaya ya Magharibi kisiwani Zanzibar wakiwa na taulo za kike walizopatiwa na Shirika la Bima Zanzibar ( ZIC) kama sehemu ya kusherehekea siku ya wanawake duniani