Na.Mwandishi wetu,Timesmajira
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo, amesema Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji na Shirikisho la Urusi ili kuongeza fursa za masoko, teknolojia na maendeleo ya viwanda kwa manufaa ya pande zote mbili.
Ameyasema hayo jana tarehe 9 Julai 2026, alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Urusi yaliyofanyika kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba).

Amesema Maonesho ya Sabasaba yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kukuza diplomasia ya uchumi kwa kuwakutanisha wafanyabiashara, wawekezaji na taasisi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Ameongeza kuwa ushiriki wa Urusi katika maonesho hayo unaakisi uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili na unafungua milango ya ushirikiano mpana zaidi wa kibiashara.

Aidha, amewahimiza wafanyabiashara na wawekezaji kutumia fursa zinazopatikana kupitia Maonesho ya Sabasaba kujenga ubia, kubadilishana uzoefu na kuanzisha miradi yenye tija itakayochochea ukuaji wa biashara, viwanda na uchumi wa Tanzania kwa ujumla.



More Stories
SMAUJATA waipongeza HGWT kupambana na Ukatili Mara
FCC yajipanga kuendelea kulinda ushindani maslahi ya walaji
Tututuba ahimiza matumizi ya Taasisi rasmi za fedha