Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Serikali ya Tanzania imekamata tani 356 za dawa za kulevya kuanzia mwaka 2017 hadi 2021.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Gerald Kusaya alipozungumza na wanahabari kuhusu mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara.
“Mamlaka toka kuanzishwa kwake mwaka 2017 hadi kifikia mwishoni mwa Septemba 2021 kwa kishirikiana na vuombo vingine vya dola ilifanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 45,784 wa dawa za kulevya, kilogramu 356,563.1 za dawa za kulevya pamoja na kuteketeza ekari 628.75 za mashamba ya bangi,” alieleza.
Akitoa ufafanuzi, Kusaya ameitaja bangi kuongoza katika orodha ya dawa za kulevya zilizokamatwa.
“Dawa za kulevya zilizokamatwa ni kilogramu 1,125.41 za heroin, kilogramu 26.67 za cocaine, kilogramu 199,740 za bangi, kilogramu 97,640 za mirungi, kilogramu 57,600 za kemikali bashirifu na kilo 431.02 za methamphetamine,” amearifu.
More Stories
CCM inabebwa na kazi nzuri za Rais Dkt. Samia-Makalla
Wananchi Babati wamshukuru Rais Samia kwa kuwafungulia barabara
Rais Samia aungwe mkono ajenda ya nishati safi ya kupikia