May 2, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bakwata yawahimiza Watanzania kuendelea na maombi ya mvua ya kheri

Na Mwandishi wetu

MUFTI Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewasisitiza wa Waislamu wote na Watanzania kwa ujumla kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu ili aweze kuendelea kutoa mvua kwa kipimo sadifu kisicho ambatana na madhara wala maafa pamoja na kutulida dhidi ya maradhi mbalimbali ikiwemo UVIKO 19

Akizungumza na waandishi habari Jijini Dar es salaam kwa niaba ya Mufti Mkuu Tanzania, Msemaji wa Mufti Sheikh Hassan Chizenga amesema Novemba 17 mwaka huu Mufti Mkuu wa Tanzania aliwangiza waumini nchini kufunga siku tatu na kuomba dua kwa wingi kutokana na mvua kuchelewa mno kunyesha nchi nzima .

Amesema wito huo uliitikiwa na mikoa yote ambapo dua za kumbelembeleza zilifanyika na hatimaye Mwenyezi Mungu aliweza kujibu dua hizo bila ya madhara yoyote.

“Nawaomba waislamu wote na Watanzania kwa ujumla tuendelee kumuomba Mungu atupe mvua hizi kote ambako zimefika na sehemu ambazo bado hazijafika ziweze kufika kwa kipimo sadifu”amesema Chizenga

Na kuongeza kuwa Mungu hufulaia pale mwanadamu anapomuomba hivyo nawaomba tuendelee kumbembeleza kwa dua”alisisitiza

Vilevile amesema hotuba za ijumaa za wiki pamoja na Shughuli za kiibada zijikite zaidi katika kumshukuru Mungu kufanya hivyo Mungu atasikia kilio na kujibu kwa haraka katika kipindi hiki ambacho wema wa duniani ni wachache na uovu umekithiri.

Pia amesema kumshukuru Mungu kutaifanya aione nchi ya Tanzania ikivuma sauti za kumsifia na kumshukuru ili azidi kuipenda Tanzania na kuizindishia neema nyingi.

Sheikh Chizenga amesema kutokana na neema kubwa watanzania na waislamu kwa ujumla wanapaswa kutambua kuwa Mungu yupo na ndiye mtawaka wa dunia hivyo yapasa kujipendekeza kwake kwa ibada nyingi kisha kutubu makosa.

“Tukiomba toba kutatusaidia kupata neema nyingi mbalimbali tunazoziitaji katika maisha yetu duniani na kesho Ahkhera”amesema

Anaongeza kuwa Mungu anasema katika Qurani tukufu aya 10 hadi ya 12 anasema na kutuhusia kupitia kinywa cha Nabji Nuhu kwa kusema na kusema muombeni msamaha mola wenu katika yeye ni mwingi mno wa kusamehe.

Sheikh Chizenga amesema kitu cha muhimu zaidi katika dua na ibada ni kuzidi kujinyenyekeza kwa Mungu ili azidi kudumisha amani nchini na kuwashika mkono viongozi wa nchi .