December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tanzania, Kenya, Uganda mwenyeji Afcon 2027

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limezipa Tanzania, Kenya na Uganda uenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Pamoja na kuzipa nchi hizo za Afrika Mashariki uenyeji wa AFCON ya 2027, Rais wa CAF, Dk. Patrice Motsepe ameitaja Morocco kuwa mwenyeji wa AFCON ya 2025.