January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TANESCO yahamasisha wananchi kuunganishiwa umeme

Na Magesa Magesa, TimesMajira Online, Rukwa

SHIRIKA la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Rukwa
limeendelea kufanya uhamasishaji na utoaji elimu kwa wananchi wa
Vijiji vilivyopitiwa na Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA) awamu
ya tatu mzunguko wa kwanza ambapo wanavijiji hao wamepoangeza juhudi za shirika hilo

Wananchi wengi wa vijiji vilivyopitiwa na mradi wamehamasika juu ya
huduma za umeme na kulipia kuunganishwa umeme wakati wa kampeni hiyo ya utoaji elimu na uhamasishaji wateja.

Mtaalamu kutoka ofisi ya uhusiano na masoko Siliveta Matiku akizungumza na wananchi waliopitiwa na mradi wa umeme mkoani Rukwa wakati wakiwahamisha wananchi kujiunga na huduma ya umeme.Pcha zote na
Magesa Magesa

Kampeni hiyo imeendeshwa na wataalamu kutoka Kitengo cha Masoko
TANESCO kwa ushirikiano na Ofisi ya Mkoa wa Rukwa kupitia kwa
wataalamu mbalimbali wa masoko na uhusiano kwa wateja.

Uhamasishaji huo uliwezesha vijiji zaidi ya 25 vilivyoko wilaya za Sumbawanga,Laela,Kalambo na Nkasi kupata elimu kuhusu manufaa ya umeme na huduma za shirika.

Mmoja wa wataalamu hao Sylivesta Matiku kutoka kitengo cha Masoko ,ameeleza kuwa uhamasishaji wa huduma ya umeme na utoaji wa elimu umewezesha wananchi wengi kujua taratibu za kuunganisha umeme, elimu ya usalama,ulinzi wa miundombinu,tahadhari ya ajali za umeme,
elimu ya matumizi bora ya umeme na jinsi ya kujiepusha na vishoka.

Wananchi wakisiliza elimu inayotolewa kuhusiana na faida za kujiunga na mradi umeme wa REA ulipotia kwenye maeneo wanayoishi.

“Miongoni mwa Vijiji vilivyonufaika na elimu hizo ni Kaengesa,
Lyapona, Mpombwe, kapozwa, kalambo,kilewani, kalemashi, katili
kipanga, vingine vitakavyonufaika ni kazovu, korongwe, kabwe, mbende,katani, Zimba, Nankanga, kizumbi, mpui, miangalua,Lowe, kalambezi,Tunko,Kianda, Lowe” amesema Matiku.

Kwa upande wa Afisa Uhusiano kwa Wateja Mkoa wa Rukwa Saidy Mremi amesema kuwa, mradi wa umeme wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza umeunganisha vijiji 120 na huduma ya umeme Mkoani humo.

Aidha mradi huo umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 wananchi
wanaokadiriwa kuunganishwa ni wateja zaidi ya 3500 kwa umeme wa njia moja na tatu.