Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeelezea kusikitishwa na baadhi ya watu wasiofahamika ambao waliwasha moto na kuunguza nguzo nne za umeme katika eneo la Gera Kashasha wilayani Muleba,Kagera.
“TANESCO tunatoa taarifa kuwa, watu ambao bado hawajafahamika wamewasha moto uliosababisha kuungua kwa nguzo nne za kusafirisha umeme eneo la Gera Kashasha wilayani Muleba.Tukio hilo limesababisha baadhi ya maeneo Wilayani Muleba kukosa huduma ya umeme,”imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO makao makuu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wakati wataalamu wa TANESCO na mafundi wakiendelea na kazi ya kurejesha huduma ya umeme, TANESCO kwa kushirikiana na vyombo vya usalama inaendelea na uchunguzi ili kuwabaini na kuwafikisha kwenye vyombO vya sheria wale wote waliohusika.
“TANESCO inatoa wito kwa wananchi kushiriki katika ulinzi wa miundombinu ya umeme.Tafadhali usiguse wala kukanyaga waya uliokatika au ulioanguka chini, toa taarifa ofisi za TANESCO zilizo karibu nawe.Wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo, Kitengo cha Miito ya Simu 0222194400 na 0768 985100,”imeongeza taarifa hiyo
More Stories
Mpogolo amahukuru Dkt Samia
PPRA yatakiwa kuwa mfano kusimamia uadilifu Serikalini
Kamati ya Kudumu ya Bunge yaridhishwa ujenzi soko la Kariakoo