May 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TAKUKURU yafanikiwa kuzuia hujuma mradi wa barabara

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma imefanikiwa Kuzuia njama za hujuma za utumiaji nondo zisizokiwa na ubora katika mradi wa barabara ya mzunguko wa nje (Ringroad) kutoka Nala-Vyeyula-Ihumwa-Bandari Kavu yenye kilomitw 52.3.

Hayo yamesemwa Leo Agosti 23 mwaka huu na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma John Joseph huku akisema zoezi hilo limefanikiwa kwa kushirikiana na  kushirikiana na mkandarasi mshauri anayetekeleza mradi huo.

Aidha amesema katika kuhamasisha jamii kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa kupitia programu ya TAKUKURU Rafiki katika Kata ya Chigongwe wilaya ya Dodoma iliwezesha kurejeshwa kwa Mota ya kusukuma maji yenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili Laki Tatu na Elfu Hamsini ambayo ilikuwa imeibiwa.

“Muhusika ambaye aliiba Mota hiyo licha ya kujulikana lakini hakuwa amechukuliwa hatua na viongozi wa kijiji hali iliyopelekea wananchi kukosa huduma ya maji katika kata hiyo” amesema Mkuu huyo.

MKUU wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma John Joseph akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake

Katika hatua nyingine amesema vipaumbele vyao kwa mwezi April 2023 mpaka Juni 2023 ni wamepanga kufanya uchunguzi katika tuhuma zilizoainishwa katika taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali na tuhuma zingine kadri zitakavyobainika.

kwa.mujibu wa Joseph jukumu la uzuiaji rushwa wamefanya tafiti kumi (10) katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo na pia wameweza kufanya warsha Kumi na tatu (13) ambazo zilitumika kuwasilisha matokeo ya chambuzi za Mifumo zilizofanyika kwa lengo la kushirika jamii..

“Katika kipindi hiki maazimio Kumi na moja (11) kati ya kumi na tatu yaliweza kutekelezwa na taarifa zake za utekelezaji kuwasilishwa TAKUKURU. Vile vile tumefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo Sitini na Nne (64) katika mkoa mzima yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni Kumi na mbili” amesema..

Aidha, Mkuu huyo ametoa wito kwa wananchi wote wa jiji la Dodoma kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa kwani mapambano dhidi ya rushwa ni wajibu wa kikatiba wa kila mmoja wetu.

“Tukumbuke pia kuwa rushwa ni adui wa taifa letu kama ilivyo ujinga,maradhi na umasikini na ikumbukwe kuwa rushwa ni chanzo kikubwa cha umasikini yaani ni adui anayechochea na kuchechemua maadui wengi” amesema.

Amesema katika jukumu la uzuiaji rushwa wamefanya tafiti kumi (10) katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo na pia wameweza kufanya warsha Kumi na tatu (13) ambazo zilitumika kuwasilisha matokeo ya chambuzi za Mifumo zilizofanyika kwa lengo la kushirika jamii.

“Katika kipindi hiki maazimio Kumi na moja (11) kati ya kumi na tatu yaliweza kutekelezwa na taarifa zake za utekelezaji kuwasilishwa TAKUKURU. Vile vile tumefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo Sitini na Nne (64) katika mkoa mzima yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni Kumi na mbili” amesema.