Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Moshi
MWENYEKITI wa BAWACHA Taifa, Sharifa Sulleman, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuandika historia ya kuunganisha Taifa ambalo lilikuwa limegawanyika vipande vipande.
Sharrifa ametoa kauli hiyo kupitia hotuba yake ya BAWACHA kwenye kongamano la Siku ya Wanawake Duniani, ambapo Rais Samia alikuwa mgeni rasmi.
Anaona dhamira yake ya kuunganisha taifa la watu wenye uzalendo kwa nchi yao iendelee.
Amesema amefurahi kwa kuweza kujionea umahiri wa wanawake wa CHADEMA kwa macho yake kwani ni jeshi lenye uwezo na udhubutu usiotiliwa shaka.
Amesema wanatambua kwamba uchaguzi mkuu wa 2020 haukuwa uchaguzi, bali ulikuwa uchafuzi uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Amesema pamoja na uchaguzi huo kuwa uchafuzi, lakini wanawake hao walisimama imara na kuweza kutangaza na kutolea mfano jimbo la Nkasi. Aidha amesema katika uchaguzi huo wanawake 62 wa CHADEMA waligombea ubunge,Baraza la Wawakilishi 10, udiwani 207 na idadi hiyo itaongezeka kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
More Stories
Serikali yahimiza wananchi kutembelea vivutio vya utalii
Magunia ya kufungia tumbaku yakamatwa
Madereva 16,Mwanza wafungiwa leseni ya udereva