Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbeya
TAASISI ya Tulia Trust Jijini Mbeya imesema kuwa taasisi hiyo imeweka mikakati ya kuendelea kuwasaidia wazee wasiojiweza katika kupata matibabu katika hospitali mbalimbali pindi wanapopatwa na maradhi
Akizungumza na Timesmajira leo kuhusu mikakati ya taasisi hiyo katika kuwasaidia wazee wasiojiweza Jijini hapa Ofisa habari wa Taasisi ya Tulia Trust , Joshua Mwakanolo amesema pia taasisi hiyo katika kuadhimisha siku ya wazee duniani kila mwaka wamekuwa wakifanya masuala mbali mbali yanayohusu wazee ikiwa ni pamoja na kufahamu changamoto mbalimbali wanazokutanazo katika jamii.
Aidha Mwakanolo amesema kuwa pia mikakati ya taasisi hiyo kuendelea kutoa misaada kwa wazee wote wa mkoa wa Mbeya wasiojiweza ikiwa ni pamoja kuwafikia wazee wote kutoa misaada ,uhitaji wazee ,kujua idadi ya wazee wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na kuangalia uhitaji mkubwa unaotakiwa kwa wazee wote.
“Lakini pia tuna wazee zaidi ya ( 6000 )kwa mkoa wa mbeya wamekatiwa bima ya afya ili waweze kupatiwa matibabu katika hospitali mbali mbali ,huu utaratibu huwa tunaufanya kila mwaka kwa hiyo toka tulipoanza mpaka leo tuna wazee zaidi ya (6000 )ambao tunawahudumia kwasababu tunamiini kuwa suala la afya ni changamoto kubwa kwa wazee ”amesema Mwakanolo.
Hata hivyo Mwakanolo amesema katika kuwatambua wazee taasisi hiyo ina mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba ili kuweza kuwatambua wazee wasiojiweza ,na pia alitoa wito kwa jamii kuendelea kushikamana ili kuweza kuwasaidia wazee .
Aidha Afisa habari huyo amesema kuwa mpaka sasa wameweza kuwasaidia wazee 1,0000 vitu mbali mbali ikiwemo vyakula , mavazi na mwaka huu tutaendelea kuwaona tena wazee hawa kwasababu wengine hawana uwezo kabisa wa kutembea inabidi wawafuate kwenye makazi yao kuwasaidia.
John Edward ni mzee aliyenufaika na bima amesema kwamba bima hiyo imekuwa msaada mkubwa kwake kutokana na kuumwa mara nyingi maradhi mbali mbali .
Taasisi ya tulia Trust inayoongozwa na Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Akson ambayo imekuwa ikijishughulisha katika kazi mbali mbali za kijamii ikiwemo mikopo kwa wajasiliamali .
Mzee Greyson Mwakyulu amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa wazee hasa upande wa bima ambazo zimekuwa zikiwawezesha kupata matibabu pindi wanapoumwa.
“Sisi Wazee hatuna cha kusema kuhusu Taasisi hii ya Tulia truist inayoongozwa na Spika wa bunge na Mbunge wa jimbo la Mbeya kwani sisi wazee na umri wetu huu tunakuwa na maradhi mengi sasa ukiwa huna bima na unachangamoto ya kutokuwa na kipato wala ndugu wa kukusaidia hali inakuwa ngumu sana kwetu sisi wazee ,tunaomba wadau na taasisi zingine zituone kwa kutusaidia mahitaji mbali mbali ya kujikimu kwani wen gi wetu tuna changamoto nyingi hasa ukizingatia maisha yetu sisi wazee ni magumu “amesema mzee huyo.
Mnufaika mwingine ambaye ni mzee Christina Ngaya mkazi wa Majengo amesema kwamba kwa muda mrefu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu na kifua lakini baada ya kupatiwa bima imekuwa msaada kwake na hivyo kupata matibabu kwa wakati tofauti na awali alipokuwa hana bima alikuwa anaugua nyumbani bila kupata matibabu kutokana na kukosa msaada kuishia kuguulia nyumbani .
Kwa upande wake Meneja wa Taasisi ya Tulia Truist ,Jackline Boaz amesema kuwa katika kuhakikisha wazee wote wanafikiwa taasisi hiyo kumekuwa kukifanyika jitihada za kila namna ili kuwafikia wazee hasa wale ambao hawana uwezo kabisa wa kutembelea .
“Taasisi ina timu kubwa ya vijana hawa wanachofanya ni kufika maeneo yote ambako wazee wanaishi kujua idadi yao ili kupata orodha ya kuweza kuwasaidia vitu mbali mbali na huo ni mwendelezo wetu ambao taasisi imekuwa ikifanya kila mwaka hata kabla ya maandalizi ya maadhimisho ya siku wazee duniani “amesema Meneja huyo.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja