January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Taasisi ya TEMDO yatengeneza vifaa tiba kuipunguzia serikali gharama.

Na Zena Mohamed, Timesmajiraonline, Dodoma. 

TAASISI ya Uhandisi na Usanifu Mitambo (TEMDO),ambayo ipo chini ya Wizara ya viwanda na biashara ,imesemema imeanza kutengeneza vifaa tiba nchini baada ya kugundua serikali inatumia fedha nyingi kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi.

Hayo yamesemwa  jijini hapa leo na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko wa Temdo,Dk.Sigisbert Mmasi katika Tamasha la karibu Dodoma linaloendelea katika viwanja vya chinangali.

Amesema kuwa Temdo wameona wanaweza kutengeneza vifaa tiba ndani ya nchi na hadi sasa wameshatengeneza vifaa tiba 15 ambavyo vipo tayari kutumika katika hospitali  mbalimbali nchini.

Alitaja baadhi ya vifaa tiba hivyo kuwa ni machera,stendi ya kuwekea dripu,loka,vitanda vya kufanyia oparesheni na vitanda vya kuzalia mama wajawazito ambavyo vyote vimeanza kutengenezwa.

“Hii ni kutokana na Temdo kuangalia kila sekta ndio maana kwenye sekta ya afya pia tumetengeneza mashine kwajili ya kuchoma takataka za Hospitali ambayo inaweza kuchoma takataka hadi kwenye joto la 1200,huku primari ukichoma kwa joto la 600 na tukumbuke unapochoma takataka za Hospitali  unatakiwa usitumie joto la chini kwasababu ni hatari zaidi,”amesema.

Aidha amesema serikali Temdo kwa lengo la kuhudumia Tanzania nzima na inauwezo huo na mtu akija kwao wanamuelekeza na teknolojia namna ya kutumia mashine zinazotengenezwa hapo.

Hata hivyo Mmasi alitaja majukumu ya Temdo kuwa ni kubuni,kusanifu na kutengeneza mashine au teknolojia kwajili ya kusaidia viwanda vidogo,vikubwa na vya kati.

Pia ameeleza kazi zilizofanywa na Temdo hadi sasa na kusema wameshatengeneza viwanda vitano ambavyo vinamashine ya alizeti kuanzia kuchakata mbegu hadi kusafisha mafuta,kiwanda cha siagi ya karanga,kiwanda chenye mashine za unga wa lishe ambazo zinadraya na mtambo wa kutengeneza kuni mbadala.