January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Spurs kumpiga chini Mourinho isipofuzu Ligi ya Mabingwa

LONDON, England

KLABU ya Tottenham imetajwa kumfuta kazi meneja wakeJose Mourinho ikiwa klabu hiyo itashindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mwaka wa pili mfululizo.

Mourinho, mwenye umri wa miaka 58 raia wa Ureno, alichukua nafasi ya Mauricio Pochettino mnamo Novemba 2019 wakati Spurs ikishika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini England.

Hata hivyo, Spurs wanakabiliwa tena na matarajio halisi ya kumaliza nje ya nne bora. Wanashika nafasi ya saba katika jedwali la Ligi Kuu msimu huu wakiwa wamebakiza michezo saba tu na wamesalia na alama ya sita kwa nafasi ya nne West Ham.

Ligi Kuu ya Mabingwa huleta mapato mengi kwa vilabu kuliko Ligi ya Uropa na Spurs wanahitaji kuhakikisha mapato yao yanabaki juu kusaidia kufadhili gharama ya uwanja mpya wenye thamani ya Pauni moja.

Mourinho anaweza kutoa kombe la kwanza kwa Spurs katika miaka 13 ikiwa timu yake itashinda kwenye fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Manchester City baadaye mwezi huu, lakini haiwezi kuficha ukweli kwamba wamepungukiwa na kiwango kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

%%%%%%%%%%%