March 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Singida wadhamiria makubwa utunzaji wa mazingira

Na Bashiri Salum,TimesMajira Online,Singida

WANANCHI mkoani Singida wameaswa kutumia mbinu mbadala za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na athari za mabadiliko ya tabianchi ili kupata mazingira safi na kuondoa uwezekano wa kupata upungufu wa chakula katika ngazi ya kaya.

Viongozi mbalimba wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani singida wakiwa wamejipanga wakisubiri zoezi la upandaji wa miti

Mbinu hizo zimetajwa kuwa ni upandaji wa miti ili kutunza Mazingira na kuleta mvua pamoja na kilimo cha uwele na mtama aina ya Serena hasa katika kipindi hiki ambacho Mamlaka ya Hali ya hewa imebainisha kwamba mvua zitanyesha chini ya wastani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa upandaji miti ngazi ya mkoa uliofanyika katika pembezoni mwa ziwa Kindai na Munangi Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Pasksi Muragili ambaye amemuwakilisha RC Singida katika kazi hiyo amesema ili kupambana na changamoto ya mabadiliko ya Hali ya hewa lazima kila Kaya ipande miti kuanzia miwili katika maeneo yao na kwa wakulima walime mtama aina ya Serena ili kujipatia chakula cha kutosha.

Amesema ilikuwa utaratibu wa Mkoa kufanya usafi kila Siku ya Jumamosi lakini kwa sasa usafi huo utafanyika kila Siku huku Jumamosi ikitumika kama Siku ya kupanda miti mpaka mvua itakapofikia kikomo.

Mkuu wa Wiliaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili akimwagilia mti alioupanda kando ya ziwa kindai wakati wa uzinduzi wa upandaji miti uliofanyika hivi karibuni katika manispaa hiyo.Picha zote na Bashiri Salum

DC Muragili amefanya kwamba ni jukumu la kila mtu, Halmashauri na Manispaa mbalimbali hapa Singida kuhakikisha miti inapandwa inalelewa na inalindwa dhidi ya mifugo na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema ya utunzaji wa mazingira.

Akizungumza kuhusu usafi mgeni rasmi huyo amesema kuanzia sasa Manispaa ianze kuwashughulikia wote ambao watatupa takataka hovyo badala ya kutumia vizimba vilivyotengwa maeneo mbalimbali ya mjini.

Aidha, DC Muragili akaagiza kila mkulima ahakikishe analima ekari moja anayoipanda mtama aina ya Serena kwa kuwa unastahimili ukame na unatoa mazao mengi, mazao mengine ni kama uwele huku alisisitiza watu kufanya kazi kwa bidii.

Naye Kaimu Mkuu wa Idara ya Mazingira Shuku Kaishwa akitoa taarifa yake kwa mgeni rasmi amesema ni mpango wa Manispaa kuhakikisha kila Taasisi inapewa eneo la kudumu la kupanda miti na kuitunza ili kuifanya Singida kuwa ya kijamii.

Mkurungezi wa Manispaa ya Singidau Zefrin Lubuva akishiriki upandaji miti zoezi lilofanyika hivi karibuni katika eneo la ziwa kindai  lengo likiwa ni utunzaji wa mazingira .

Aidha Shuku amebainisha kwamba kupitia Manispaa wameandaa Mpango wa kuhamasisha jamii na taasisi kuanzisha mashamba ya miche pamoja kueleza jamii faida zitokanazo na mazao ya miti pamoja na upandaji wa miti aina ya mihimbo katika vyanzo vya maji.

Afisa mazingira huyo ametoa wito kwa jamii ya wafugaji na wataalamu wa mifugo kuendelea kuielimisha jamii juu ya ufugaji wa ndani (zero Grazing) ili kuepuka kusambaza kwa mifugo nje na kujaribu miti iliyopandwa huku akiwataka wananchi kuhamasika na kuanza kutumia nishati mbadala ambao utapunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wakuu wa idara mbalimbali ngazi ya mkoa na Halmashauri,kamati ya ulinzi na usalama, taasisi mbalimbali watumishi wa umma wanafunzi na wananchi mbalimbalme