Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
LICHA ya kutoka suluhu ya bila kufungana katika mchezo wa marudiano wa Ligi Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United ya Nigeria, klabu ya Simba imefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo kwa ushindi jumla wa goli 1-0 walioupata katika mchezo wa awali wa ugenini uliochezwa wiki iliyopita kwenye uwanja wa New Jos.
Katika mchezo huo wa awali goli pekee la Simba lilifungwa na kiungo Mzambia, Clatous Chama akimaliza kazi nzuri iliyofanywa na Winga Luis Miquissone.
Sasa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) watakutana na FC Platinum ya Zimbabwe ambayo imetinga hatua hiyo baada ya kuwafunga Costa do Sol ya Msumbiji kwa ushindi wa jumla ya goli 4-1 baada ya kushinda 2-1 na kisha kushinda goli 2-0 katika mchezo wa marudianoa uliochezwa leo kwenye mji wa Bulawayo.
Katika mchezo huo, Simba itaanzia ugenini katika mchezo utakaochewa kati ya Desemba 22 au 23 katika uwanja wa National Sport na kisha watarudiana kati ya Januari 5 au sita katika uwanja wa Mkapa.
Simba waliingia wakihitaji ushindi ambao ungewafanya kusonga katika hatua ya pili (32 bora) huku Plateau United wakitaka kulipa kisasi kwa Simba ambao walifunga katika ardi yao ya nyumbani katika mchezo wa kwanza.
Hadi dakika ya 20 ya mchezo huo, Simba walikuwa wameshafika mara kadhaa langoni mwa wapinzani wao huku Muzamiru Yassin akikosa bao baada ya kupaisha mpira juu ya lango alimalizia pasi ya Nahodha John Bocco.
Simba waliebdelea kufanya mashambulizi katika lango la Plateau ambao walionekana kuwa na utulivu lakini nao wakijibu mashambuli kwa Simba lakini hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyoweza kupata bao.
Kipindi cha pili Plateau walionekana kubadilika na kucheza mpira wa kasi na kufany mashambulizi kadhaa langoni mwa Simba ambao walionekana kutochgeza mpira wa kasi kama ilibyokuwa kipindi cha kwanza.
Kusaka goli kwa wachezaji w Pleteau kuliwafanya kucheza madambi mengi na kuwapa faida Simba ambao hawakuweza kutumia vema nafasi hizo ikiwemo mipira 11 ya kona walizozipata na mchezo huo kumalizika kwa suluhu.
More Stories
Watumishi wa Fahari wafanya Bonanza
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship