
Na Israel Mwaisaka, Rukwa
Silaha moja ya kivita aina ya AK-47 pamoja na risasi 23 imesalimishwa kwa hiari na mtu au watu wasiofahamika katika Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa Rukwa. Usalimishaji huu umetokana na elimu inayoendelea kutolewa kupitia kampeni ya usalimishaji wa silaha haramu.
‎Silaha hiyo imesalimishwa Oktoba 19, 2026, katika eneo la wazi la Kijiji cha Lyazumbi, Kata ya Paramawe, ikiwa ni sehemu ya mwitikio wa wananchi katika kuunga mkono kampeni ya usalimishaji silaha haramu iliyozinduliwa Agosti 31,2026 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Patrobas Katambi.
‎Kampeni hiyo inaendelea kuhamasisha wananchi kusalimisha kwa hiari silaha wanazomiliki kinyume cha sheria kabla ya kuhitimishwa kwa kipindi cha msamaha Oktoba 31, 2026.

‎Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, SACP Shadrack Masija, anawasisistiza wananchi kusalimisha silaha wanazomiliki kinyume cha sheria.
‎Aidha, anawahimiza pia wamiliki wa silaha zilizosajiliwa kisheria ambao wamefariki dunia, wazee sana au wasiokuwa na uwezo wa kuendelea kuzitumia kutokana na umri mkubwa au maradhi, kuzisalimisha kwa ajili ya usalama wa jamii.

More Stories
Mabaki ya mkonge kuzalisha chakula, mbolea
Mbeya UWSA yatii agizo la Waziri Aweso
Madiwani viti maalumu jiji la Mbeya wakabidhi msaada wa chakula shule ya msingi Kambarage