May 15, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule ya Sekondari Benjamini wajivunia mafanikio

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa Wilayani Ilala wanajivunia mafaniko Kitaaluma kila mwaka inafanya vizuri .

Hayo yalisemwa na Mkuu wa shule ya Benjamini Mkapa Joseph Deo, wakati wa Mahafali ya 22 ya kidato cha nne.

Mwalimu Deo amesema shule ya Sekondari Benjamini mkapa ilizinduliwa 1998 shule ya kutwa yenye Mchanganyiko Wavulana na Wasichana yenye Wanafunzi kidato cha kwanza mpaka cha sita pia ina Wanafunzi wenye Ulemavu wa ngozi ,Viungo uono hafifu na viziwi wapatao 168.

“Mafanikio Kitaaluma shule ya Sekondari Benjamini Mkapa ni mazuri miaka mitatu mfurulizo Wanafunzi Wangu wanafanya vizuri mwaka 2019 ufaulu kidato cha sita asilimia 99 mwaka 2020 asilimia 98 mwaka 2021 asilimia 100 mwaka 2022 asilimia 99.3 tuna ushirikiano mzuri baina ya Wazazi ,Walimu na Wanafunzi ” amesema Deo .

Aidha Mwalimu Deo amesema matokeo ya kidato Cha nne mwaka 2018 ufaulu asilimia 80 Mwaka 2019 ulikuwa asilimia 89 mwaka 2020 asilimia 96 mwaka 2021 ulikuwa asilimia 97 .3

Mwalimu Deo alisema wanajitaidi Ili kufikia lengo la kufuta ziro za daraja la nne kwa Wanafunzi wote wa kidato cha nne

Alisema kidato cha pili matokeo yake mwaka 2018 asilimia 95 mwaka 2019 asilimia 98 mwaka 2021 ufaulu asilimia 99.2 shule ina nidhamu nzuri Wanafunzi kwa ajili ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya walimu wafanyakazi wasio walimu ,Wazazi ,Wanafunzi na uongozi wa Shule .

Mafanikio mengine shule ya Benjamini Mkapa imefanikiwa kuwa na Wanafunzi walioshiriki kuandika INSHA mbalimbali na kuwa washindi pamoja na washindi wa Mazingira mshindi wa kwanza kwa shule za Serikali 2022 wametunukiwa tuzo ya ushindi .

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam Donatus Richard ,alisema Elimu ni ufunguo wa maisha Adui namba Moja Umasikini ,Maradhi na Ujinga Elimu ya Tanzania ni Bora amewataka Wazazi kuwasomesha watoto hapa nyumbani wasikimbilie nje .

Richard amesema NMB ni Benki kubwa matarajio tutapata wafanyakazi Bora amewataka wawe waminifu wakianza kazi baada kumaliza masomo waje kutumikia Taifa .

Aliwataka Walimu kufanya kazi kwa bidii na juhudi kwani kazi yao ni wito wafanye kazi kwa weledi katika kujenga Taifa .

Amewapongeza Shule ya Benjamini Mkapa kwa kufanya vizuri Kitaaluma na kufanikiwa kupata mafanikio makubwa sekta ya Elimu .

Meneja Richard amesema Benki ya NMB ni sehemu ya Jamii Kila mwaka inatenga asilimia Moja kusaidia Jamii katika maswala ya afya ,Elimu kuhusu changamoto za Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa watazitatua kwa kufuata Taratibu .

Mwalimu Joseph Deo wa Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa Wilayani Ilala akikabidhi Risala Kwa meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam Donatus Richard katika mahafali ya 22 ya shule hiyo.
Mkuu wa shule ya Sekondari Benjamin Mkapa Mwalimu Joseph Deo akisoma risala katika mahafali ya 22 ya Sekondari Benjamini Mkapa