May 15, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TRA yaanza kampeni ya mlango kwa mlango Simiyu

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) leo imeanza kampeni yake ya Elimu ya mlango kwa mlango katika mkoa wa Simiyu wilaya ya Bariadi yenye lengo la kuelimisha wafanyabiashara juu ya masula mbalimbali ya Kodi sambamba na kusikiliza changamoto zao ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

Mkuu wa wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange amesema amefurahishwa na ujio wa Maafisa hao katika wilaya hiyo ambayo itawapa fursa wafanyabiasha kuuliza maswali na kutoa maoni.

“Nawaomba wafanyabiashara wote wa wilaya hii mtoe ushirikiano kwa maafisa hawa pindi watakapo watembelea katika maduaka yenu kwani hii ni fursa nzuri kwenu kuuliza maswali na kutoa maoni yenu”amesema

Na kuongeza kuwa
“Nawashukuru sana maafisa wa TRA kwa kuja kutetembelea katika kipindi hiki ambapo wilaya ya Bariadi imekua ikipiga hatua ya maendeleo makubwa na matumaini na kuendelea kulipa kodi zaidi”.

Aidha aliwasisitiza wafanyabiashara wa Wilaya hiyo inayoongoza kwa makusanyo katika mkoa wa Simiyu kuendelea kulipa kodi kwa hiari bila ya kushurutishwa ili kuweza kuisadia serekali kukamilisha miradi ya kuwaeletea maendeleo ya nchi.

Pia aliwakumbusha wafanyabiashara hao kuendelea kutoa risiti kila wanapuza bidhaa au kutoa huduma na wananchi kudai risiti kila wanaponunua bidhaa.

Kwa upande wa Ofisa wa Kodi kutoka kitengo cha Elimu na Huduma kwa Mlipa kodi Mkoa wa Simiyu, Benjamin Makobwe amesema lengo la Kampeni hiyo ni kutoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara sambamba na kusikiliza changamoto zao.

“ leo tupo hapa mkoa wa Simiyu wilaya ya Bariadi kwa lengo la kuelimisha wafanyabiashara wa eneo hili masuala mbali mbali ya kodi pamoja kusikiliza changamoto na madukuduku yao kwa lengo kuyafanyia kazi”.

Kwa upande wao wafanyabiashara wa wilaya hio wamefurahishwa sana na kuwapngeza maafisa wa TRA kwa kufika katika wailaya ya Bariadi kwa lengo la kuwapatia elimu zaid katika masuali ya Kodi .

Alitoa wito kwa wafanyabiashara wengine kutoa ushirikiano kwa maafisa hao na kuwaahimiza wafanyabiashara kutoa risiti halali za EFD kila wanapouza na wananchi kudai risiti ili kuiwezesha serekali kukusanya kodi ambayo ndio inayotumika kujenga mashule, vituo vya afya, barabara na usamabazaji wa maji mijini na vijijini.

Naye mfanyabiashara Faida Jishiku amesema amefurahishwa na ujio wa maafisa wa TRA kwani wamekuwa wakifanya kazi kwa pamoja katika kurahisisha ukisanyaji wa Kodi.

Kampeni ya Elimu ya mlango kwa mlango huendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) chini ya kitengo cha Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa kuwatembelea wafanyabiashara wa mikoa yote nchini kwa lengo kuwapatia elimu ya kodi pamoja kusikiliza changamoto zao pamoja na maoni na kuyafanyia kazi ili kujenga mahusiano mema na wafanyabiashara na kurahisisha ulipaji wa kodi bila ya kukwaruzana.