November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule ya Msingi Yangeyange Msongola wajivunia Mafanikio

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Shule ya Msingi YangeYange iliyopo Msongola Wilayani Ilala imejivunia mafanikio kitaaluma katika sekta ya Elimu kwa kufanya vizuri kila mwaka .

Mwalimu Mkuu wa Yangeyange Abraham Gabriel, aliyasema hayo katika mahafali ya nne ya Darasa la Saba yaliofanyika katika ukumbi wa Santiago Msongola Wilayani Ilala .

Mwalimu Gabriel alisema katika shule yake mwaka huu ni mahafali ya nne shule yake ilianza 2016 ,shule hiyo Ina wanafunzi Mchanganyiko ikiwemo Wanafunzi wa kitengo cha Elimu Maalum cha walemavu wa akili ,kituo cha Memkwa na darasa la awali hadi la Saba ambapo jumla ya Wanafunzi 3683.

Mwalimu Gabriel alisema kati ya Wanafunzi hao wavulana 1801 na Wanafunzi wasichana 1862 na Walimu idadi yao 34 Wanaume Saba na Wanawake 27 .

“Shule yangu tunajivunia mafanikio kila mwaka tunafanya vizuri kitaaluma katika MATOKEO kwa kila mwaka wanafaurisha Wanafunzi asilimia 100 wote wanaenda Sekondari kutoka na ushirikiano mzuri baina ya Wazazi Walimu na wanafunzi” alisema Gabriel .

Mwalimu Gabriel akizungumzia Wanafunzi wa darasa la Saba wanaomaliza alisema wameandaliwa vizuri kitaaluma Darasani wameandaliwa vizuri kutokana na Mazingira ya shule ya kujisomea yapo vizuri na MATOKEO yao ya mitihani ya Moko ,Moko mkoa na Moko Wilaya na Kata kwa shule za Serikali wamefanya vizuri wameshika alama za juu.

Mwalimu Gabriel aliwaasa Wazazi kuwa elimu ya Msingi ndio mwanzo wa elimu baada kumaliza darasa la Saba wanaenda Sekondari na chuo amewataka huko wanapokwenda wawe na nidhamu Ili waweze kusonga mbele elimu msingi walilelewa kama yai hivyo Wazazi wasimamie ipasavyo Ili wasiingie katika makundi hatarishi .

Mwenyekiti wa CCM kata ya Msongola Mwita Mahando, alipongeza mafanikio ya shule hiyo na kuwataka Wazazi kujenga mahusiano na Walimu huku akiwataka wafuatilie Maendeleo ya watoto wao shule.

Mwenyekiti wa CCM Mwita katika upande mwingine aliwataka Wazazi kuwalinda watoto wao wa kike na wakiume wasimamie sekta ya Elimu Ili iweze kuwasaidia baadae kwani Elimu aina mwisho vijana ni nguvu kazi ya Taifa la kesho .

“Nawaomba Wazazi tuunge mkono Ilani ya Chama cha Mapinduzi sekta ya Elimu ,Elimu Bure kazi yetu Wazazi ni kununua sare za Shule na madaftari Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeondoa ada kuanzia Elimu Msingi dhumuni lake kuwataka watoto wasome kwa bidii waweze kuendeleza “alisema Mwita .