May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule ya Jema Kindergarten wafanya ziara maktaba ya Taifa

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Shule ya Jema Kindergarten wamefanya ziara ya kimasomo kujifunza katika Maktaba ya TAIFA wilaya Ilala mkoa Dar es Salaam sehemu ya utaratibu waliojiwekea shule hiyo wakati wa likizo ya masomo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa shule ya Jema Kindergarten Maria Lucas, alisema dhumuni la ziara hiyo ya kimasomo ili watoto waweze kujifunza utamaduni wa nchi yetu katika maktaba Serikali .

“Wanafunzi wa Jema Kindergarten leo wamefanya ziara yao ya kimasomo katika utaratibu wa shule tulijiwekea Wanafunzi kazima wawe na ziara ya kimasomo kwa ajili ya kujifunza mazuri yanayofanywa na nchi yetu ya Tanzania katika uongozi wa Dkt .Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. “alisema Maria .

Maria Lucas ,alisema katika maktaba ya Taifa kuna vitabu vya Wanafunzi wote vya kujisomea ambapo wanafunzi wa Jema Kindergarten leo wamejisomea na kujifunza .

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dkt.Samia kwa kuboresha maktaba hiyo ya Taifa kuwa ya kisasa ambapo pia ameweza kujenga maktaba ya watoto na za wakubwa.

Maria aliomba jamii na Wanafunzi, kujengaTabia ya kufanya ziara na kujifunza katika maktaba ya TAIFA kwani kuna vitabu mbalimbali.

Muhutubi wa Watoto Maktaba ya TAIFA Lilian Dalola, alisema Kitengo chao wanapokea Watoto kuanzia miaka sifuri na kuendelea katika maktaba ya kisasa ambayo ina kila kitu.