May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule ya Benjamini yajivunia ongezeko la ufaulu

Na Heri Shaaban , TimesMajira Online

SHULE ya Sekondari Benjamini William Mkapa , wajivunia mafanikio ya ufaulu kitaaluma ndani ya miaka mitatu wameshika alama za juu katika matokeo ya kidato cha sita .

Akizungumza katika mahafali ya ishirini na nne ya shule hiyo Mkuu wa Shule ya Benjamini William Mkapa Joseph Deo, alisema mwaka 2021 matokeo ya kidato cha sita asilimia 100 ,mwaka 2022 matokeo asilimia 99 mwaka 2023 matokeo asilimia 99 inayokana ma jitihada za Walimu wa shule hiyo na wanafunzi ambapo mwaka huu 2024 wanaondoa Division O ikiwezekana kupata Division one 150 au zaidi.

“Tunajivunia ufaulu wa miaka mitatu mfululizo katika shule yetu tumefanya vizuri jitihada za walimu wangu na wanafunzi na sasa tumejipanga kuondoa Division O mikakati yetu kupata Division one 150″alisema Deo .

Deo alisema nidhamu ya Wanafunzi wa Shule ya Benjamini Mkapa ni nzuri inatokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Walimu na Wafanyakazi wasio Walimu ,Wazazi na wanafunzi na uongozi wa shule katika kuendelea maendeleo ya shule hiyo.

Alisema pamoja na Changamoto mbalimbali zilizopo nidhamu nzuri ni kichecheo kikubwa kwa maendeleo ya kitaaluma katika shule hiyo.

Aidha alisema mazingira bora ya kujifunzia na kusomea katika shule hiyo yanafanya waongeze ufaulu kila mwaka kutokana na kuweka mazingira ya shule vizuri iliyopelekea kupata ushindi wa kwanza wa mazingira kwa shule za Sekondari za mjini kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo.

Pia wameboresha miundombinu ya shule ikiwemo vyoo pamoja na mitaro ya kusafirishia maji machafu ambayo ilikuwa hatarishi kwa wanafunzi na watumishi.

Akielezea mafanikio mengine alisema wanaendelea na ukarabati kadri wanavyokusanya fedha kutoka Mradi wa Elimu ya Kujitegemea (E/K) pamoja na fedha zinazotolewa na Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Zainabu Mbiro Mkuu wa Wilaya Msaafu, alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza sekta ya Elimu nchini kwa kujenga shule za sekondari na Msingi ikiwemo kuboresha miundombinu ya elimu na wanafunzi wanasoma.

Zainabu Mbiro alisema pia Rais Dkt Samia ameboresha mikopo ya Elimu ya juu kwa wanafunzi wa vyuo kwa sasa wanakopa mikopo hiyo ya vyuo kwa kufuata Taratibu.

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu na Diwani wa Gerezani Fatuma Abubakari kwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi vizuri ndani ya jimbo la Ilala na kata ya Gerezani.

Katika hatua nyingine alipongeza uongozi wa shule ya sekondari Benjamini William Mkapa kwa kukuza taaluma shuleni na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.

Zainabu aliwataka wahitimu wa shule ya Benjamini William Mkapa wawe na maadili mazuri kwa yale waliofundishwa shuleni hapo huko wanapoenda wawe mabalozi na kuitangaza Shule ya Benjamini William Mkapa.