January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shija Richard kuwania Jimbo la Mbagala

Na Mwandishi Wetu

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Mbagala Shija Richard amechukua fomu ya kuwania kiti hicho.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Temeke Richard alisema lengo kuu ni kushirikiana na wana-Mbagala katika kuwaletea maendeleo .

Amesema kuwa anahitaji kushirikiana Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta maendeleo kwa wana Mbagala na taifa kwa ujumla.

Richard alisema pia atahakikisha anaisimamia ilani ya chama cha Mapinduzi katika utekelezaji.