Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ametoa maelekezo matano katika utekelezaji wa kiasi Cha Shilingi Bilioni 64.9 kilichopokelewa na Wizara hiyo kutoka kwenye fedha za UVIKO 19 ikiwemo kuhakikisha miradi yote iliyopangwa inakamilika kabla au ifikapo Mei 30 mwakani.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prpofesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza na waandishi wa habari jijiji hapa kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19 katika Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ambayo imepata shilingi bilioni 64.9.
Profesa Ndalicako ametaja maeneo mengine kuwa ni kuimarisha Elimu ya mafunzo na ufundi stadi na kuimarisha Mazingira ya elimu ya ualimu na kuongeza idadi ya walimu.
Amesema katika maeneo hayo matatu wataongeza uwiano wa vitabu Ili kusaidia wanafunzi wenye uoni hafifu na wasioona ,kununua vifaa saidizi ,kujenga mabweni katika chuo cha ualimu Morogoro
Aidha amesema,ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ,ni lazima maandalizi yote yanayohusu Fedha hizo yakamilike ifikapo Octoba 30 Mwaka huu lakini pia matokeo ya utekelezaji wa mradi yaendane na thamani ya fedha zilizotengwa,na vifaa vyote vinunuliwe kwa bei ya soko .
Aidha,amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo aandae mfumo mahsusi wa uratibu,ufuatiliaji na utekelezaji wa mradi ili kubaini changamoto na kuzitafutia ufumbuzi na kutolewa taarifa za utekelezaji kila mwezi.
“Kwa pande wa Wizara mpango huu utanufaisha maeneo mbalimbali ikiwemo kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maaulm ambapo shilingi bilioni 1.4 zimtengwa ,utaimarisha elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi ambapo kiasi cha shilingi bilioni 57.9 kimetengwa lakini pia utaimarisha mazingira ya utoaji elimu ya ualimu ambapo shilingi bilioni 5.4 kimetengwa.”amesisitiza Profesa Ndalichako
Akifafanua zaidi Profesa Ndalichako amesema,athari za VIKO 19 zilichangiwa na changamoto zilizopo katika mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ,uwiano wa mindombinu kwa wanafunzi na walimu na uchache wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia katika taasisi za elimu.
“Kutokana na changamoto hizo namshukuru sana mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ,Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kwa kuipa kipaumbele sekta ya elimu katika kutatua changamoto hizo.”
Profesa Ndalichako ametumia nafasi hiyo kuwataka wasimamizi wote wa miradi katika Wizara hiyo kuhakikisha inatekelezwa kwa ubora unaotakiwa na kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa ilingane na thamani halisi ya fedha.Â
More Stories
Wanafunzi 3000 wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Mkutano Mkuu maalumu CCM wapitisha Rais Samia ‘mitano tena’
Dkt.Kikwete:Ushindi wa CCM ni lazima