Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online,Dar
SERIKALI imepongeza kampeni ya usafi inayotekelezwa na Shirika laMaendeleo la Ujerumani (GIZ) kupitia mradi wake wa DeveloPPP ambapo limepanga kuwafikia watu 25,000 kwenye Mkoa wa Dar es Salaam.
Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Wilaya ya Temeke, Ally Hatibu, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usafi ni afya katika Wilaya hiyo kwenye hafla iliyofanyika Mbagala, kampeni inayotekelezwa na Shirika la Emmanuel Borotherhood Foundation (EBF) na BINGWA Laboratories.
Hatibu aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo, alisema kampeni hiyo yenye lengo la kudhibiti magonjwa yatokanayo na uchafu kwa mama na bba lishe, makondakta na madeveva wao na madereva wa bajaji italeta manufaa makubwa kwa jamii.
Mradi wa usafi ni afya unaofadhiliwa na Wizara ya Maendeleo ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Ujerumani unatekelezwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kupitia mradi wake wa Developpp.
Hatibu alisema Wilaya hiyo inachangamoto mbalimbali za magonjwa yatokanayo na uchafu lakini ingawa serikali imesogeza huduma za afya karibu na wananchi na kuboresha upatikanaji wa dawa bado magonjwa hayo yanagharimu fedha nyingi kwa serikali na familia.
Amesema kampeni hiyo italeta ufumbuzi wa changamoto hizo kwani mbali ya kutoa elimu ya usafi walengwa watapewa bidhaa mbalimbali za usafi ikiwemo sabuni za kunawa mikono, vitakasa mikono, dawa za kuulia vijidudu vya magonjwa ya kuambukiza .
“Ninawapongeza sana kwa kuendesha mradi huo na napenda kuwahakikishia kuwa serikali ya awamu ya sita itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kama ilivyo kwa GIZ kuwawezesha wananchi kujikwamua katika changamoto za afya,” amesema
Msemaji wa GIZ, Lesue Stephen amesema shirika hilo linaungana na serikali na wadau wengine kuhamasisha jamii kupitia kampeni ya usafi ni afya ili kuchochea mabadiliko ya tabia chanya ya kujijali kimwili na usafi wa maeneo ya kazi na mazingira ya nayotuzunguka.
“Leo hii tunafurahi kujumuika nanyinyi hapa Mbagala lakini kampeni hii itaendelea na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam ikilenga watui 25,000 hasa walioko katika misongamano kama masoko na vituo vya usafiri kwa kufanya kampeni ya kutoa elimu ya kuzuia magonjwa ya kuambukiza,” ameema
Amesema bidhaa ambazo zimekuwa zikitumika kwenye kampeni hiyo zimetengenezwa na makampuni ya kitanzania kama BINGWA Laboratories na AFRICRAFT hivyo kuwanufaisha kwa kipato wajasiriamali wadogo zaidi ya 100 wengi wao wakiwa ni wanawake.
“GIZ tunapenda kusisitiza kwamba elimu itakayotolewa kwenye kampeni hii ikawe chachu kwetu sote kuendeleza tabia ya kudumisha usafi na kujijali ili kujikinga na magonjwa ya kuambukiza. Pia kwa wale watakaopata vipeperushi wavisome na kuwapa taarifa ndugu na jamaa kuhusu kujikinga na magonjwa,” amesema
More Stories
Watakiwa kushirikiana kutikomeza matatizo ya lishe
CCBRT yazidi kuunga mkono juhudi za Rais Samia
Madaktari bingwa wa Samia watua Rukwa