May 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yaombwa kuweka barabara na umeme Nyang’hwale

Na David John,timesmajira online

MENEJA wa Mgodi wa EBR and partners uliyopo kijiji cha LYULU kata ya LYULU wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita Sunday Tumaini amesema tangu walipofika kijijini hapo mwaka 2016 na kuanza shughuli za uchimbaji wa kati Kijiji kimekuwa kikinufaika na uzalishaji unaotokana na Mgodi huo.

Amesema kuwa kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo hilo kulikuwa na wananchi ambao pia walikuwa wanafanya shughuli hizo na kwa kuliona hilo Mkurugenzi wa Mgodi huo akawakatia sehemu ya kipande kilichopo ndani ya leseni yake ili nao waendelee na shughuli za uchimbaji wa Madini ya dhahabu kwa lengo la kujipatia kipato na Serikali kunufaika.

Sunday ameyasema hayo hivi karibuni mbele ya waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali waliotembelea mgodi huo kwa lengo la kujifunza na kuripoti habari zinazohusiana na madini.

Nakuongeza kuwa Tumewekeza kwenye sekta hii ya madini ila changamoto yetu kubwa ni miundombinu ya barabara na umeme hivyo tunaomba Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan iweze kutusaidia kutoboreshea barabara na kutuletea umeme ili tuweze kufikisha madini tunayopata Sokoni kwa urahisi”.Amesema

” Ndugu zangu wanahabari kama mnavyoona hii ni baadhi ya mitambo ambayo tunaitumia kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu hapa na kwakweli Mgodi huu umekuwa na tija sana hususani kutokana na uzalishaji wake kwani wananchi wameweza kupata ajira lakini pia Serikali imekuwa ikifaidika na kile ambacho linatoka hapa.”amesema Tumaini

Ameongeza kuwa umeme utawezesha kuongeza uzalisha kwa tija na serikali kuendelee kunufaika kutokana na uwekezaji wao kwa kuweza kutoa miraaba mikubwa na hata wananchi wanaozunguka eneo la mgodi waweze kunufaika kupitia mgodi huo.

Katika hatua nyingine wanamshukuru Afisa madini mkazi (RMO) wa mbogwe kwa ushirikiano mkubwa anaowapatia ukiwemo ushauri mzuri ambao kimsingi unawasaidia kwenye shughuli zao mfano uliwezesha kukaa na mkurugenzi nakuona Kuna umuhimu wa kuwapa wanakijiji leseni ya Iparan’ombe ili weweze kuchimba.

Amefafanua kuwa wachimbaji hao wadogo waliwapa utaratibu wa uchimbaji mdogo wa madini kuwa watakuwa wanakatwa mawe wanayokuwa wamepata kupitia uchimbaji wao ikiwemo asilimia za mraaba wa serikali na mawe mengine yanabaki kwa muwekezaji.

Ameongeza kuwa na asilimia nyingine wanayopata wanarudisha kwenye jamii inayowazunguka hivyo wao wanachukua asilimia 30 na wachimbaji wanachukua asilimia 5 ila wanapata manufaa makubwa kupita uwepo wa mgodi huo kwasababu kwenye duara moja wanatoa mifuko ya mawe zaidi ya 400 na maduara yapo zaidi ya 20.

Akizungumzia faida za uwepo wa Mgodi huo Tumaini amesema wamekwangua barabara kutoka wilayani kuja kijijini hapo na wameweka molamu na kwa kufanya hivyo kumekuwako na mawasiliano mazuri kati ya kijiji na wilayani maana watu wanapita bila shida ila hofu iliyopo ni nyakati za Masika ndio maana wanaomba serikali iwe kusaidia.

Amesema wao kama.mgodi bado wako karibu na wananchi kwenye shughuli za maendeleo ambapo katika siku za hivi wameweza kusaidia kuezeka shule ya Msingi Bea baada ya upepo kuharibu paa ambapo uongozi wa kijiji ulikwenda kuomba msaada na wao kuweza kusaidia kupaua shule hiyo na michango mingine midogo midogo wanasaidia sana.