Na Rose Itono, TimesMajira Online, Dar
SERIKALI imetaka maboresha ya mahusiano yaliyofanywa na Shirika la Posta Tanzania na benki ya CRDB katika huduma za kifedha yanawafikia watanzania wengi ili kuhakikisha Tanzania unafikia uchumi wa kidigitali.
Akizindua huduma za CRDB wakala katika ofisi za Shirika la Posta Waziri wa Mahusiano na Teknolojia ya Habari Dk. Faustine Ndugulile amesema fedha ni kichocheo muhimu katika maendeleo ya hivyo kuna kila sababu ya kutanua wigo wa hiduma za kifedha.
Dkt.Ngudulile amesema bado takwimu zetu za matumizi kwenye mfumo rasmi wa huduma za kifedha ni mdogo hivyo mahusiano hayo yahakikishe watanzania wengi zaidi wanaingia kwenye mfumo huo.
“Kwenye mfumo rasmi wa guduma za kifedha ni mdogo kwani asilimia 16.7 wanapata huduma za kifedha kupitia benki,asilimia 48.6 wanapata huduma za kifedha kupitia simu za mkononi,asilimia 6.7 haijulikani wanapata huduma kupitia mfumo gani na huku asilimia 28 hawana huduma hiyo”amesema Dk.Ngugulile na kuongeza kuwa mahusiano hayo yawafikie kwa kuwarasimisha watanzania kwenye mfumo rasmi wa fedha.
Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kufanya uwekezaji katika sekta ya mawasiliano ambapo bajeti ya mwaka 2021/22 imetenga sh. Bilioni 300 kwa ajili ya kuboresha huduma na kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kidigitali.
Pia amelipongeza shirika hilo kwa kuanzisha huduma ya pamoja ambayo itarahidisha huduma mbalimbali za kiserikali kwa wakati mmoja pamoja na kuanzisha duka mtandao na watanzania kupata fursa ya kuuza bidhaa zao ndani na nje ya nchi.
Naye, Kaimu Posta Masta Mkuu Macrice Mbodo alisema shirika limeazimia kuhudumia wananchi na kuchagiza maendeleo ya kiuchumi.
Amesema shirika hilo limeunganisha zaidi ya ofisi 350 nchini pia lipo katika Umoja wa Posta Duniani (UPU)lenye matawi zaidi ya 670,000 duniani.
Kwa upande wake Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara kutoka shirika hilo Costantine Kasese alisema mbali na kutoa huduma xa kifedha shirika linatoa huduma ya usafirishaji wa barua,vifurushi na sampuli kwa ajili ya kupeleka kwa mkemia.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Abdulmajid Sekela alisema atahakikisha mawakala wanafanya kazi kwa ueledi na kuwapatia mafunzo ili kuboresha utendaji kazi wao na wananchi kupata huduma bora.
More Stories
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania