Na Rose Itono, TimesMajira Online
SERIKALI imeutaka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kuhakikisha inajumuisha na kuimarisha kaya za watu wenye ulemavu Ili kuwezesha kundi hilo kupata maendeleo
Akizungumza kwenye mkutano wa Kikao kazi Cha wadau kwaajili ya kupokea maoni kuhusu ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye mpango wa kunusuru kaya za walengwa Mkurugenzi wa Idara ya Watu wenye ulemavu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Suzana Mayengo alisema ujumuishaji na uimarishaji kwa watu wenye ulemavu utaliwezesha kundi hilo kupata maendeleo na kuondokana na umasikini
Alisema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa awamu ya Sita Dkt. Samia Suluhu Hassan Iko mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wake wanaondokana na umasikini sambamba na kushiriki Shughuli mbalimbali za maendeleo
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Ladislaus Mwamanga alisema lengo kubwa la kikao ni kupokea maoni kuhusu ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye mpango wa kunusuru kaya za walengwa
Alisema TASAF itahakikisha ushirikishwaji kaya za watu wenye ulemavu kwenye mpango wa kunusuru kaya za walengwa unahusisha nchi nzima Tanzania Bara na Zanzibar
Alisema serikali kupitia mpango huu imeamua kutoa ruzuku Maalumu kwa kaya za watu wenye wenye ulemavu Ili kuwaongezea uwezo wa kufanya majukumu yao.
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania Ernest Kimaya ameshukuru serikali kwa kushirikisha watu wenye ulemavu kwenye mpango huu ambapo kwa sasa kundi hilo limekuwa likiweza kutoa mchango kwa familia zao
Hata hivyo ameionba serikali kuangalia namna ya kusaidia kundi la watu wenye ulemavu kwenye nafasi za ajira pindi fursa zinapopatikana.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango