November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yaendelea kushirikiana na wadau kukabiliana na majanga

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Serikali kupitia mwaka wa fedha 2023/24 imeendelea kushirikiana na wadau wa nje na ndani ya nchi kuhakikisha kwamba uwezo wao wa kukabiliana na majanga mbalimbali ikiwemo majanga ya asili kama vile matetemeko na mafuriko yanaboreshwa na hivyo kuendelea kuikinga nchi.

Aidha kupitia idara ya menejimenti ya maafa imeendelea kukabiliana na majanga nchini na kutoa elimu kwa wananchi kuwaonyesha namna ambavyo jamii inaweza kujikinga na majanga mbalimbali.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi wakati alipotembelea na kukagua Banda la ofisi yake katika maonyesho ya 47 ya biashara ya Kimataifa (Sabasaba) .

“Ofisi ya waziri Mkuu sera Bunge na uratibu inalo jukumu la kuratibu namna ambavyo tunakabiliana na majanga katika nchi yetu hivyo kupitia idara ya menejimenti ya maafa tuko hapa kwaajili ya kutoa elimu kuwaonyesha namna ambavyo jamii inaweza kujikinga na majanga mbalimbali”

“Majanga yanaleta hasara sana katika nchi yetu, yanaweza yakaleta hasara ya maisha na mali n.k na hivyo kuathiri uchumi hivyo idara yetu inaendelea kuratibu namna ambavyo nchi yetu inajenga utayari wa kukabiliana na majanga haya lakini pia yanavyotokea namna ya kukabiliana nayo” Amesema Dkt. Yonazi

Aidha Dkt. Yonazi amesema wamewekeza katika teknolojia na sasa wana mifumo ambayo inawasaidia kwaajili ya kazi ya kukabiliana na maafa kwa kutoa viashiria vya awali lakini pia kuratibu namna ambavyo wale wanaowajibika kwenda kwenye eneo la tukio wanavyowajibika, wanavyowezeshwa na wananchi kuweza wakatoa taarifa.

“Tunayo mifumo ya kitehama ambayo inatusaidia namba 190 ambayo ikipigwa mwananchi anaweza kutoa taarifa na taarifa hiyo itafi”

Kadhalika Dkt. Yonazi amesema wanayo maono ya kufanya kwamba idara ya maafa iwe na uwezo hata kusaidia nchi nyingine zinazotuzunguka

“Tumeona kwamba majanga haya yanaweza yakakabili nchi zaidi ya moja na hivyo nchi Moja isiweze kuwa na uwezo wake binafsi wa kuweza kukabiliana na majanga hayo yanapokuwa makubwa, tunataka kuendelea kujenga uwezo ambavyo tunaweza kusaidia na nchi zingine na jambo hili litaweza kutusaidia siyo tu kujenga uwezo wa ndani lakini pia kuleta fedha za kigeni wakati ambapo inabidi”

Matukio katika picha wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi katika mabanda mbalimbali kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam .