Na Mwandishi Wetu, Timesmajiraonline,Dar es Salaam
SERIKALI imehakikisha kuwa mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) yataendelea kupewa kipaumbele, huku huduma za kinga, matibabu na upatikanaji wa dawa muhimu zikiendelea kutolewa bila kukwama licha ya changamoto zinazotokana na kupungua kwa misaada kutoka kwa wahisani wa maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa leo, Julai 9, 2026, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Winnie Byanyima, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam.

Prof. Kabudi alisema Serikali imeendelea kuwekeza katika sekta ya afya kupitia vyanzo vya ndani vya mapato ili kuhakikisha huduma zote muhimu zinazohusiana na mapambano dhidi ya UKIMWI zinaendelea kutolewa kwa wananchi bila kuathiriwa na mabadiliko ya ufadhili kutoka nje




More Stories
TARI Selian yawaalika wakulima maonesho ya Kilimo-biashara
BRELA yawapa elimu ya Urasimishaji Biashara vijana wanaoshiriki Sabasaba
Mixx, TCDC kuimarisha huduma za kifedha kwa wakulima