January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali ,wadau waombwa kuchangia vifaa kwa watoto wenye ulemavu

Na Esther Macha, Timesmajira, Online ,Mbeya

SERIKALI kwa kushirikiana na wadau wameombwa kuchangia upatikanaji wa vifaa ikiwemo baiskeli kwa watoto wenye ulemavu wa viungo na uoni hafifu katika shule msingi mchanganyiko ya  Katumba (2)iliyopo wilayani Rungwe  mkoani Mbeya .

Akizungumza na Timesmajira leo Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Katumba (2)Mauyeni kilumbe amesema kuwa   shule hiyo ina uhaba wa vifaa saidizi kwa watoto wenye ulemavu kutokana na  wengine kutambaa kutokana na ukosefu wa baiskeli.

Kilumbe ameomba wadau  kutoa misaada mbali mbali  na kusema vifaa vilivyopo havitosherezi  mahitaji ya watoto wenye ulemavu  , wengine wanatumia mashine za kuandikia za nukta nundu  , wenye uarubino wanauhitaqji wa mafuta ,kofia  na mahitaji mengine muhimu .

“Kwasasa hivi tuna baiskeli tano tu ambazo nazo hazitosherezi maana hapa tuna watoto wengine  hawawezi kutembea bila baiskeli    na `zilizopo zina uchakavu  kilichopo hivi sasa tuna uhitaji wa baskeli  16 kwa watoto wenye  ulemavu wasiojiweza kabisa,ila mahitaji zaidi ni  baskeli 16, na mashine 24 za kuandikia  za nukta nundu  kwa wenye uoni hafifu , “amesema

Ameongeza kuwa “watoto watano wanatumia vibao vya kawaida hizi mashine mpya tunazofatilia tunaambiwa zimepitwa na wakati lakini kwa mpya kabisa za kisasa ni  shilingi mil.1 hivyo tunaomba wadau na jamii kujitokeza kusaidia watoto hawa “amesema Mkuu huyo wa shule .

Aidha aliomba wazazi kuzidisha upendo kwa watoto wao  wenye ulemavu  kwa  kuwaleta shule kwani  shule hiyo haina malipo yoyote na kusema kuwa kitendo cha kumficha mtoto mwenye ulemavu ndeani ni kumnyima haki ya kupata elimu .

Akizungumzia kuhusu wadau ambao wamekuwa wakisaidia shule hiyo Kilumbe amesema Child Support Tanzania kwa jitihada zake za kuhakikisha kuwa kusaidia wanafunzi wenye ulemavu kwa kutoa vifaa saidizi pamoja  na elimu na kuhamasisha wazazi wanaoficha watoto majumbani kuwapeleka shule.

Kwa upande wake Ofisa elimu Msingi  halmashauri ya Busokelo ,Atuvonwe Chaula amesema kuwa kwa halmashauri hiyo wamekuwa wakifanya jitihada za kuwatumia walimu maalum kwenda vijijini kuwatambua watoto walemavu baada ya wazazi kutambua kuwa watoto wao walikuwa wanaachwa.

Damas Mwambeja ni Mwakilishi wa watu wenye ulemavu aliwataka wadau kuendelea kusaidia shule ya Katumba (2)na kusema licha ya serikali kuwa mstari wa mbele kusaidia shule  hiyo basin a wadau na jamii wana wajibu wa kusaidia vifaa mbali mbali .