May 21, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

SERIKALI imewataka wahitimu MNMA kuwa Raia wema

Na Rose Itono

Wahitimu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) kuwa raia wema na kuendeleza maadili na uzalendo kwa mustakabali wa taifa.

Akizungumza kwenye mahafali ya 17 ya Chuo hicho Dar es Salaam mwishoni mwa wiki Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt, Francis Michael amesema sasa hivi taifa linakabiliwa na changamoto ya uvunjifu a maadili hususan kwa vijana

“Ni wazi kuwa maadili ya Sasa hususan kwa vijana yamepiromoja hivyo kutokana na hatua hiyo wahitimu mnaomaliza mkawe chachu ya kuwa mfano wa kuigwa kwa wengine Ili taifa liweze kuwa na vijana wenye maadili, amesema Dkt Michael

Dkt Michael amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa uongozi wa chuo Ili kuhakikisha changamoto zinazokikabili zinamalizika

Aidha amesema kama ilivyo utaratibu wa chuo kufundisha programu za maadili na uzalendo programu hizo zinaendelea na kila mwanafunzi anayesoma aweze kuzisoma.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Prof Shadrack Meakalila amesema Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilianzishwa kwa Sheria ya bunge namba 06 ya mwaka 2005,Chimbuko lake ni Chuo Cha Kivukoni ambacho kilianzishwa rasmi Julai 29 mwaka 1961

Prof Mwakalila amesema dira ya Chuo hicho ni kuwa kitovu Cha utoaji wa maarifa bora kwa kutoa elimu na mafunzo kuhusu ubunifu na uvumbuzi.

Amesema jukumu la Chuo ni kuendesha mafunzo ya kitaalumakatika fani ya sayansi jamii kwa kuwango Cha astashahada, shahada,shahada ya kwanza,shahada ya umahiri na shahada ya uzamivu.

Pia amesema majukumu mengine ya Chuo ni kuendesha mafunzo ya elimu ya kujiendeleza, kufanya utafiti,kutoa ushauri wa kitaalamu katika sekta ya umma na sekta binafsi sambamba na huduma kwa jamii.

Amesema Chuo kimekuwa na mafanikio mbalimbali ikiwepo ongezeko kubwa la udahili sambamba na miradi mbalimbali ya kimaendeleo

Amesema palipo na mafanikio changamoto hazikosekani hivyo kwa sasa Chuo kinakabiliwa na changamoto kuu mbili ikiwepo ya ufinyu wa baheti na upungufu wa wafanyakazi katika idara za uendeshaji na Taaluma ukilinganisha na uhitaji.

Amesema Chuo kimeanzisha miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikiigharamia kupitia asilimia 40 ya mapato yake ya ndani lakini kiadi Cha fedha kinachohitajika kwenye miradi ni kikubwa hivyo miradi imekuwa ikikwama hivyo anaiomba Serikali kuashika mkono Ili kufanikisha

Jumla ya wahitimu 5,480 wamehitimu mafunzo Yao kwa mwaka wa masomo 2021/2022 ambapo kati yao wanawake ni asilimia 55 huku wanaume ni asilimia 44,9.