May 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

SBL kuwapa mihela mashabiki kupitia kampeni ya ‘Maokoto chini ya kizibo’

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online, Dar es Salaam

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Limited, itatoa zawadi zenye jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa muda wa miezi 3 kwa wateja kupitia kampeni yake ya ‘Maokoto chini ya kizibo’.

Kampeni hiyo itakayowalenga wateja nchini kote, imezinduliwa Oktoba 16 mwaka huu, katika ukumbi wa Kitambaa Cheupe Lounge, Sinza jijini Dar es Salaam, na inatarajiwa kudumu mpaka Desemba, 2023.

Pia, kampeni hiyo inatoa fursa kwa kampuni kuwashukuru wateja wake na kuwataka kuendelea kufurahia bidhaa zake.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa East African Breweries Limited (EABL), Jane Karuku amesema zawadi watakazotoa zitawapa furaha wateja pamoja na fulsa ya kujipatia kipato.

“Tunajivunia kutoa zawadi za kusisimua ambazo sio tu zitaleta furaha lakini pia kutoa frusa ya kujipatia kipato. Zawadi mbalimbali za kifedha zitanufaisha idadi kubwa ya wateja, hatimaye kuwasaidia watu wengi zaidi kuwa na kipato kwa muda mrefu.

Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi, amesisitiza, “Maokoto chini ya Kizibo” inasukumwa na azma ya kuibua hisia za furaha na kusaidia maisha ya wateja wetu, na nia ya kuacha alama muhimu kwa kuleta sababu za kusherekea kila mahali, na kujitolea kwetu kwa namna ya kipekee kusaidia jamii yetu”.
 

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa SBL, Anitha Rwehumbiza, ameongezea kuwa kampeni hiyo itafanyika kwa muda wa miezi mitatu wakiwa wameandaa zawadi zenye thamani ya TZS Bilioni 1.5.

“Tutakuwa tunatoa zawadi za TZS 4M kila wiki na zawadi nyinginezo za papo kwa hapo kila watakapokuwa wananunua bidhaa zetu mbalimbali kama vile Serengeti Premium Lite, Serengeti Premium Lager, Pilsner, Guiness Smooth, na Smirnoff Ice Black”.

William Lyimo, maarufu kama ‘BillNass’, mwanamuziki mashuhuri katika Tasnia ya burudani Tanzania na balozi wa kampeni hiyo, amesema amefurahi sana kuona SBL ikiwa na dhamira nzuri kwa wateja wake.

“Nimefurahia dhamira ya SBL katika kuleta furaha na kusaidia maisha ya wateja wake. ‘Maokoto chini ya Kizibo’ inaburudisha, hata kwa masharti yake, tayari unaweza kujionea namna ilivyopokelewa vizuri sokoni,” amesema mwanamuziki huyo.

SBL inalenga kuonyesha upendo na shukrani kwa wateja wake waaminifu huku ikiwataka kuendelea kufurahia bia yenye ubora wa hali ya juu.

Katika wiki zijazo, SBL inakusudia kuwazawadia wateja wake na ofa za kusisimua, mashindano na zawadi, ikitoa fursa ya kushinda zawadi za kuvutia na kufurahia kumbukumbu za aina yake.