January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

SBL kuendelea kuchangia maendelea ya michezo

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imesema itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha na kuchangia sekta ya michezo hapa nchini ambayo pia inaajiri Watanzania wengi hasa vijana kupitia shughuli mbalimbali zilizopo ndani ya sekta hiyo.

Kwa muda mrefu sasa, Serengeti imekuwa mdau mkubwa wa maendelea ya michezo na imekuwa ikifadhili michezo mbalimbali ikiwemo soka, riadha na mchezo gofu.

Mkuu wa kitengo cha Bia wa SBL, Anitha Msangi aliuambia Mtandao huu kuwa, kampuni hiyo inatambua mchango wa michezo na kwamba kupitia chapa ya Serengeti imekuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo ya michezo.

“Ni kupitia chini ya udhamini wa bia ya Serengeti Lager, timu ya Taifa Taifa Stars iliweza kufuzu mashindano makubwa kabisa barani Afrika ya Kombe Mataifa ya Afrika (AFCON) yaliyofanyika nchini Misri mwaka 2019 ikiwa ni miaka 39 tangu ifuzu kwa mara ya mwisho,”.

Kabla ya kufuzu mashindano hayo makubwa barani Afrika, SBL kupitia kinywaji chake cha Serengeti Lager ilisaini mkataba wa miaka mitatu na TFF ambapo ilitoa kiasi cha shilingi billion 2.1 kuidhamini Taaifa Stars katika kipindi cha miaka mitatu udhamini ambao ulikuwa na mafanikio makubwa kwa timu hiyo.

Mwezi Octoba mwaka 2020 Bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) iliingia makubaliano na kusaini mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya kuidhamini Timu ya Taifa, Taifa Stars kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.

Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Wallace Karia amesema, SBL kupitia chapa ya Serengeti imekuwa ni mfano wa kuigwa katika kuchangia maendeleo ya michezo na kuyataka makampuni mengine kuiga mfano.

Mkataba huo unaogharibu shilingi bilioni 3 za Kitanzania, umesainiwa baada ya ule wa awali uliosainiwa mwaka 2017, kufikia ukomu kati kati ya mwaka huu huku timu ikijivunia mafanikio mengi katika kipindi cha udhamini.

Akizungumzia huhusu udhamini wa Taifa Stars Anitha amesema, “tunaamini kuwa kwa kuiunga mkono timu ya Taifa siyo tu tunachangia katika maendeleo ya michezo hapa nchini lakini pia kuongeza hamasa kwa mchezo wa mpira wa miguu ambao unapendwa sana na maelfu ya Watanzania,”

SBL kupitia bia ya Serengeti Lite pia imekuwa mdau mkubwa wa soka la wanawake. Mwaka 2018 Serengeti Lite ilitiliana saini na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambapo kampuni  hiyo ilitoa kiasi cha shilingi milioni 450 kwa ajili ya kudhamini ligi hiyo. Kupitia udhamini huo, Serengeti Lite inakuwa mdhamini wa kwanza kugeukia ligi ya wanawake ambayo umaarufu wake unakuwa kwa kasi.