December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Samia atunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, Uturuki

CHUO Kikuu cha Ankara, kimemtunua Rais Samia Suluhu Hassan Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Uchumi kwa kutambua uongozi wake wa kipekee katika kuendeleza mageuzi ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ambayo yameboresha ustawi wa jamii.  

Rais Samia alitunukiwa shahada hiyo ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) leo na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki, Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo jana.