Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online,Mwanza
MENEJA RUWASA Wilaya ya Misungwi,Mhandisi Marwa Kisibo amesema ndani miezi mitatu watakuwa wameshughulikia changamoto zilizojitokeza katika mradi wa maji Mbarika-Misasi,ili wananchi waweze kupata huduma ya maji.
Ambapo ujenzi wa mradi huo ulianza mwaka 2014 na ulitarajiwa kukamilika 2019 lakini hadi sasa mradi upo kwenye hatua za majaribio kutokana na kujitokeza kwa changamoto ya mabomba kupasuka wakati wakifanya majaribio.
Mhandisi Kisibo amebainisha hayo wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Veronica Kessy na Kamati ya ulinzi na usalama ya kutembelea miradi mikubwa inayotekelezeka na serikali katika Wilaya hiyo ikiwemo mradi huo.
Amesema,mradi huo ulikadiriwa hadi kukamilika kugharimu bilioni 6.3 hadi sasa zimeisha tumika bilioni 4.8 na umefikia asilimia 95 asilimia 5 zilizobaki ili mradi ukamilike ndio inaletwa na changamoto ya majaribio ya kuwa kila wanapo fanya majaribio maeneo fulani bomba zinaachia kwenye maungio(joint).
Malengo yao kama wilaya ndani ya miezi mitatu ijayo watakuwa wameweza kutatua changamoto hiyo sababu fedha tayari wanazo na wanaweza kununua valvu.
“Tumekubaliana baada ya eneo lile lililoachia na limerekebishwa sasa tusitishe majaribio ili tufunge sectional valvu kila kijiji au kila tenki ili tuweze kubaini eneo lenye changamoto kubwa maana mara nyingi tunapofanya majaribio,eneo dogo la Kasololo ndipo panapotokea uvujaji wa maji,”amesema.
Mhandisi Kisibo amesema,mradi huo ulitembelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na changamoto hiyo ndio ziliainishwa,timu ya wataalamu ili kuja na ikakubaliana kujenga tenki la kupunguza mgandamizo katika mlima wa Mambali.
“Tenki hilo tayari tumeisha likamilisha tangu Aprili na tumefanya tena majaribio lakini tunapata tena changamoto ya uvujaji maji katika eneo la Kasololo,changamoto kubwa ni kwamba mradi huu kwa urefu wake wa Km 49 una section valvu moja tu kwaio tunajikuta wanapopata changamoto tunamwaga maji karibia kwenye mradi mzima,”amesema Mhandisi Kisibo.
Hivyo amesema,mradi unatarajiwa ukikamilika utahudumia wananchi 41,539,vijiji 11 vitanufaika ambao una matenki ya kuhifadhia maji manne na bomba kuu renye urefu upatao Km 49.2 huku Km 19 ni bomba za usambazaji.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Veronica Kessy amesema,waliamua kama kamati ya ulinzi na usalama Wilaya kuweza kupita katika miradi mikubwa inayotoa huduma kwa wananchi ndani ya Wilaya ya Misungwi.
Kessy amesema,katika mradi wa Mbarika-Misasi walikuta mradi huo ulianza mwaka 2014 na ulitakiwa ukamilike 2019 lakini mpaka sasa hivi eneo hilo kwa awamu hiyo ya tatu wananchi bado hawajaweza kunufaika na mradi huo.
Amesema,changamoto kubwa ilizopelekea ni namna mkataba ulivyoendeshwa kwa maana Mkandarasi aliyekuwa site kuna vitu vingine alivifanya na mabomba mengine yalikuwa chini ya kiwango kwaio imechelewesha mradi huo kuendelea kufanyiwa uthamini mara kwa mara.
Kwa upande wake mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Sumbugu hayo Masuli Ndassa amesema,wanachangamoto ya maji tangu mwaka 1974, wanawake wanahangaika na maji ya kuchota na ndoo,wanatumia umbali mrefu wa takribani masaa mawili kufuata maji katika kisima kilichopo kijiji kingine.
“Tuliambiwa tunajengewa tenki,tutapata maji lakini mpaka leo hakuna maji,changamoto kubwa ikifika kiangazi tunahangaika sana,ni kilio kweli ombi kwa serikali ituletee maji tunasumbuka sana maana tangu 1974, tunategemea kisima kimoja na watu tumeongezeka tumezidi kisima,”amesema Ndassa.
More Stories
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi