Na David John, Timesmajira online, Mbeya
JESHI la Polisi mkoa wa Mbeya limesema kuwa tangu kuanza kwa maonyesho ya kitaifa ya nanenane Julai 28 mwaka mapaka yanakwenda vizuri na hiyo nikutoana na jeshi hilo kufanya kazi kwa mashirikiano na asasi nyingine za kiusalama.
Amesema kuwa kuna vyombo vingine wanashirikiana navyo ikiwa pamoja na wananchi wenyewe wanashirikiana na kwamba kila mtu anayeonekana kwenye kibanda anaulizi ambao ameweka kwenye eneo lake hivyo amewataka wanambeya kuwa wasifikilie kuwa mahala ambapo hawajamuona polisi wanaweza kukwapua kitu kwani lazima wajuwe kuwa kila kibanda wanachokiona kuna askari.
Kamanda Matei ameyasema hayo leo Agosti 4 jijini Mbeya mbele ya waandishi wa habari katika mahojiano maalumu yaliyofanyika kwenye viwanja vya maonyesho ya nanenane yanayoendelea jijini humo.
Amefafanua kuwa katika viwanja hivyo kuna askari wengi ambao wengine wamevalia mavazi ya kiraia hivyo wananchi lazima wajuwe kila kibanda kina ulinzi wake hivyo eneo hilo ni salama sana na tangu alivyozindua Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango na hadi alipokuwa Waziri Mkuu Mpaka hivi leo hali iko shwari kabisa.
Kamanda Matei ameongeza kuwa katika kuimarisha ulinzi kwenye jiji hilo hususani katika kipindi hiki cha maonyesho ya nanenane kuna askari kutoka Jeshi la Magereza,Jkt, kuna askari polisi kutoka idara zote nakwamba trafiki wanaongoza magari ,kuna askari wadoria na askari wa kawaida ambao wanahakikisha amani na usalama unakuwepo hivyo niwatoe mashaka wananchi
ushirikiano uliopo kati ya jeshi hilo na vyombo vingine limewahikikishia wananchi mkoani humo kuwa na amani na kuendelea na shughuli zao ikiwa pamoja na kuendelea kushiriki Maonyesho ya Nanenane bila kuwa na wasiwasi kwani ulinzi umeimarishwa kikamilifu na mtu yeyote asijalibu kufanya vitendo vya kihalifu kwani atakutana na mkono wa mrefu wa jeshi hilo.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari leo Agosti 4 jijini humo Kamanda wa Polisi mkoani humo amesema kuwa Jeshi hilo kwa kushirikiana na vyomnbo vingine vya ulinzi na usalama wamejipanga vizuri hivyo na askari wapo wa kutosha na wanafanya doria maeneo yote ya jiji hilo ikiwamo viwanja vya maonyesho ya nanenane yanayoendelea.
Kamanda Matei ameongeza kuwa hakuna shida yeyote ya usalama kwenye maonyesho hayo ya nanenane nakwamba wanakwenda vizuri kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa wa mbeya Juma Homera pamoja na kamati ya timu ya usalama ya mkoa kwaujumla wake kwani hakuna la polisi wala nini likitokea la usalama wote wanahusika yeye yupo kama mjumbe kwenye kamati ya ulinzi na usalama.
Amesema kuwa mkoani humo amani inaendelea hivyo ombi lake kwa wananchi nikutoa taarifa pale wanapoona pana kiashiria cha uvunjifu wa amani na usalama ni wajibu wao kutoa taarifa kwa askari yeyote ambaye yupo karibu na wametoa namba za simu za kwa kila mtu o715 009 931.na ya mkuu wa polisi wilaya ni 0659 888 065 mkuu wa upelelezi wa mkoa huo ni 0658 376 052 hivyo wananchi wapige na wamejipanga vizuri kumpokea rais Samia Hassan Suluhu.
Amesema Rais Samia watakuwa nayo katika mkoa huo kuazia tarehe 5,6,7 hadi 8 hivyo wamejipanga vizuri sana kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa kabisa na wananchi wanatakiwa kuendelea kuwa makini hususani barabarani wanapovuka na kutembea lazima waangalie kushoto na kulia kwani mji kwa sasa unawatu wengi na kimsingi wananchi sasa hivi wanapata kipato kwani hata nyumba za wageni zimejaa hiyo ni fursaa.
Kamanda Matei amesema kuwa kupitia maonyesho ya naenane wao kama Jeshi la Polisi wamejipanga na wanatoa elimu hususani masuala ya kinjisi watu wadawati wapo wanashughulikia ,mambo ya upelelezi kama yanakwama dawati wata wasikiliza hivyo watembelee kwenye mabanda ili kupata taarifa mbalimbali za jeshi hilo na hiyo ni pongezi kwa Rais Samia kuleta maonyesho ya nanenane mkoani humo.
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano