Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Mirerani
Royal Tour ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeendelea kuzaa matunda baada ya watalii wapatao 25 kati yao 7 ni Watanzania na kufikia jumla ya watalii 25 kutembelea Mgodi wa Kitalu C ya Madini ya Tanzanite unaomilikiwa na Kampuni ya Franone Mining Gems Ltd.
Akizungumza na vyombo vya habari, Meneja Mkuu na Mtaalam wa Miamba wa Kampuni ya Franone Mining Gems Ltd Vitus Ndakize amesema Upekee wa madini ya Tanzanite duniani umeendelea kuwa kivutio kikubwa duniani baada ya kampuni ya Franone Mining and Gems Ltd kupokea wageni hao kutoka Ufaransa.
Ndakize amesema kati ya watalii hao 18 wa Ufaransa Kuna watalaamu wa madini ajili ya kujifunza na kujionea hatua zote za uzalishaji wa madini ya Tanzanite ambayo hupatikani Tanzania pekee
Aidha Ndakize alisema kabla ya ageninhao kuwasili kitalu C katika mgodi huo, watalaamu hao wa miamba, sonara pamoja na wanafunzi wa miamba na madini wametembelea migodi ya Afrika Kusini na Ivory Coast ambako ni tofauti na Tanzania.
” Leo tuko na wageni watalii kutoka Ufaransa, kazi yao kubwa ni kutalii kwenye migodi mbalimbali duniani ,ambapo kwa Tanzania wamechagua Mgodi wa Tanzanite, hususani Mgodi wa Franone Mining Gems Ltd ndani ya ” Kitalu C” , tumeshuka nao hadi chini umbali wanMIta 800 kutoka sura ya dunia, wameona Mazingira tunayofanyia kazi na wamefurahi sana, wameongeza na Wachimbaji Kwa jinsi wanavyofanya kazi nanwaketidhika kuona jiwe ambalo linapatikana eneo hili tu kote duniani linachimbwa hapa” amesema Ndakize.
Aidha alisema lengo kubwa la ziara yao ni kuja kuona namna ya shughuli za uzalishaji wa Madini Tanzanite yanavyozalishwa, watakua mabalozi kuitangaza Tanzanite pindi warudipo Makao.
Akizungumzia utofauti na migodi mingine Ndakize amesema Kampuni ya Franone Mining Gems Ltd chini ya Mkurugenzi wake Onesmo Anderson Mbise utifauti wake Iko katika nyanja Kuu 3.
” Moja Miundombinu yake ni ya kisasa, ni Mgodi uliochimbwa kisasa yenye miundombinu ya kisasa, Mbili Mgodi huu umesheheni wataalam wote kuanzia Maijirojisti,Mining Engineering,Masavea wote wapo nanhasa Wachimbaji wakiobobea katika utaalam na tatu nmgodi wenye eneo kubwa la uchimbaji ambaouna uwezo wa kuchimba zaidi ya miaka 20 ijayo nanukawa unatoa uzalishaji ambao utaongeza mapato ya Serikali” almefafanua Ndakize.
Ndakize amesema watalii hao ndio wanunuzi wakubwa wa wa Madini aina ya Vito duniani kote likiwemo jiwe la Tanzanite, ambapo ujio wao utasaidia jiwe la Tanzanite huko duniani kote kwamba wamegika linakozalishwa na hivyo thamani nya Tanzanite inategemea itaongezeka Kwa sababu wao ni Mabalozi.
“Kitendo cha hawa watalii kufika kwenye mgodi wetu kimekuwa ni faraja kubwa sana kwani tumeweza kujifunza mengi pia kutoka kwao na tumeweza kuweka historia kwa kutembelewa na kundi hili ambalo wameweza kujionea namna ya utendaji kazi wetu”,amesema Ndakize
Ndakize ameishukuru Wizara ya Madini kwa kuwakaribisha watalii hao wa sekta ya madini kwani ujio wa wageni hao unaendelea kutangaza nchi ya Tanzania kwamba madini ya Tanzanite yanapatikana pekee nchini Tanzania na sio pengine.
Aidha ameongeza kuwa, kwa sasa mgodi huo umeshaanza kazi rasmi na wanategemea uzalishaji mkubwa kutokana na wataalamu wa miamba kutoka maeneo ambayo madini yanapatikana licha ya mgodi huo kutokufanya kazi kwa muda wa miaka mitano.
Aidha kwa upande wake Mmoja wa watalii kutoka nchini Ufaransa Camille Constant amesema amepata uzoefu wa kipekee wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite hivyo atakua Balozi mzuri kwa wenzake pamoja na watalii wengine watakao wafikishia Ujumbe kutoka Tanzania, kutoka Franone Mining Gems Ltd, juu ya Tanzanite, hakika hakuna kama Franone, hakuna kama Tanzanite.
“Nimefurahishwa sana na kuona namna ya uchimbaji wa kisasa ambao unatumika kuchimba na kupata madini ya Tanzanite ikilinganishwa na maeneo mengine walio tembelea katika nchi za Africa kusini , Ivory Cost na Ufaransa kwani nimeona utofauti mkubwa sana katika uchimbaji na nimepata uzoefu wa kutosha pia.”amesema Camille.
Hata hivyo ikumbukwe kuwa Serikali ilitangaza tenda mwaka 2022 mwezi wa wa nne ambapo kampuni ya Franone Mining Gems Ltd ilishinda tenda hiyo na mwezi wa sita na kupewa leseni ya uchimbaji mwezi wa saba mwishoni huku serikali ikiwa na ubia wa asilimia 16 na mpaka sasa umeanza kazi za uchimbaji ikitegemea kuanza uzalishaji wa madini ya Tanzanite wakati wowote kuanzia sasa.
More Stories
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa