December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rose Ree awataka wasanii kuacha Kiki

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva, Rosa Ree amewataka

wasanii wa Tanzania kuacha kiki badala yake wanatakiwa

kuamka ili sekta ya sanaa iweze kuku kimataifa.

Akiweka wazi hilo kupitia kwenye ukurasa wake wa

Instagram Rosa Ree amesema, anashangaa kuona sanaa ya

Tanzania sasa hivi imekuwa kiki au kitimu kwa kile

anachodai wasanii kununua views na mambo mengine

ambayo hayahusu.

“Ki ukweli wasanii tuamkeni, kwa sababu Nina upendo

sana na wasanii wenzangu pamoja na sanaa yetu

kiujumla. Sanaa yetu imekua ya kiki kiki, u team,

kununua views na maswala mengine ambayo hata hayahusu

sana.Tena! Msanii kama mwana sanaa na mfanya biashara

unatakiwa uzingatie “PRODUCT” unayompa “CUSTOMER”

wako.

“Mlaji ni shabiki, wewe ni mpishi sasa kwanini umpe

mlaji sanaa mavi ikiwa imepakwa asali ( ambayo ni

kiki, u team n.k) kwa juu alafu umlazimishe shabiki

ale ulichopakua.

“Tunaweka focus yetu kwa kitu ambachi sio kizuri.Na

ndio maana wenzetu wanatuacha nyuma sana!, Sijawai

kusikia mabaya ya Burma Boy, ila sasa hivi ana Grammy

na tuzo nyingine nyingi na heshima juu yake!

anaiheshimisha mpaka nchi yake! Sisi tunaheshimisha

nchi yetu kwa haya makiki?. Tunaiheshimisha nchi yetu

kwa huu uteam?, Tunaiheshimisha nchi yetu kwa sijui

kununua views youtube?, Jamani amkeni, tukifanya sanaa

legit, sanaa ambayo ni sanaa pure tutafika tunapotaka.

“Ila kama sanaaa yetu ingekua ni nguo au viatu Basi me

ningesema Ni ‘mdosho’ wa kutupa! Kinavalika lakini ni

‘fake’ sana! Na bei yake ni rahisi!, Ndio maana

wasanii wengi wanakua na ‘very short term

achievements’, na wengine wanapata majina na Zero

money. Ila ukinunua kitu original mwenyewe unajua

kabisa lazima mfuko utoboke! na hautalalamika.

“Angalia nchi zingine wanavyo Faidika kupitia sanaa.

Mtu anapata Faida na heshima juu!. Nimekutana na watu

kadhaa wa nchi za nje, wanatucheka tu!.Inasikitisha

sana,” amesema Rosa Ree.