January 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ripoti mauaji ya wanawake 2438 yazinduliwa

Na Queen Lena, Timesmajira Online,Arusha

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimefanikiwa kuzindua ripoti ya mauaji ya wanawake ambapo jumla ya wanawake 2438 wameuwawa katika kipindi cha miaka mitano 2019-2023.

Ripoti hiyo ambayo imezinduliwa Oktoba 26,2023 na LHRC imesema kuwa wanawake hao wameuwawa kwa makusudi katika kipindi hicho huku sababu zimebainika kuwa ni chanzo cha maujai hayo ni pamoja na wivu uliokithiri baina ya wapenzi,mila potofu, mali, mifumo ambayo inamkandamiza mwanamke na mambo ya kiuchumi.

Akiongea na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo katika mkutano wa Azaki na waandishi wa habari Mkurugenzi wa kituo hicho Dkt. Anna Henga amesema kuwa utafiti huo uliweza kuwahusisha wadau mbalimbali likiwemo Jeshi la Polisi kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)

Ambapo napo paliweza kuonesha wastani wa wanawake 492 waliuawa kila mwaka na wanawake 43 waliuawa kila mwezi katika kipindi hicho.

Ameendelea kwa kubainisha kuwa kwa mujibu wa ripoti iliweza kubainisha kuwasaidia mpaka kufikia Septemba 2022, tayari mauaji 472 ya wanawake yametokea ambayo ni sawa na wastani wa matukio 53 ya wanawake wanaouawa kwa mwezi kutoka wanawake 43 kuuwawa kwa mwezi.

“Hii inaashiria wastani wa ongezeko la wanawake 10 zaidi wanaouawa kwa mwezi kutoka kwa wale waliuawa katika miaka mitano iliyopita,,”.

Naye Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi kwa Mtoto dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu, Tulibake Kasongwa amesema Serikali imeweza kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa inapunguza vifo pamoja na ukatili kwa wanawake na watotoAmeeleza kuwa kutokana na jitihada hizo mpaka sasa tayari madawati ya jinsia 420 yameanzishwa katika vituo vya Polisi nchini ili kukabiliana na matukio hayo. Pia amesema kuwa kupitia madawati hayo yameweza kuzaa matunda ambapo mauaji ya wanawake kupungua kwa asilimia mbili kutoka vifo 305 hadi 298 kati ya mwaka 2020 hadi 2023.