Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.
WIZARA ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeitaka bodi ya usajili wa wataalamu wa mipangomiji kuwashirikisha wadau wote katika upangaji wa Ardhi ili kuepusha migogoro pamoja na hasara za kiuchumi na kimazingira, ambazo zinaweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa mipango hiyo.
Hayo yamesemwa jijini hapa leo na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,Ridhiwani Kikwete,akizungumza kabla ya kuzindua Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji ambapo amesema ushiriki wa wadau wengine wenye maslahi katika ardhi kwa sasa siyo wa kuridhisha sana, jambo linalosababisha maslahi yao kutozingatiwa kikamilifu kwenye mipango ya matumizi inayoandaliwa.
“Hili linajidhihirisha kwa kuwepo na migogoro mingi ya mwingiliano wa matumizi ya ardhi mijini na vijijini Migogoro hii hukwamisha shughuli nyingi za maendeleo,
“Kama inavyoeleweka, huduma za Sekta ya Ardhi hususan mipangomiji ni mtambuka kwani utekelezaji wake unagusa wadau wengi wenye maslahi juu ya ardhi,hivyo ni muhimu sana kuwashirikisha wadau kutoka sekta nyingine za maendeleo wakati wa kuandaa mipango yetu ili isikinzane na mipango ya sekta zao,”amesema.
Pia ametoa rai kwa Mamlaka za Upangaji, Wataalam wa Mipangomiji na Kampuni za upangaji kuwashirikisha wadau wote wa Ardhi
wakati wa kupanga miji na Vijiji.
Amesema kuwa wananchi lazima waelimishwe, wajue kwa undani, na wakiri kukerwa na ujenzi au uendelezaji ardhi kiholela.
“Elimu ya aina hii itawahamasisha wananchi hususan walioendeleza ardhi kiholela kuchangia gharama za uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi hasa kupitia upangaji shirikishi (urasimishaji),
“Hivyo ninatoa rai kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kutoa kipaumbele kuhusu utoaji elimu ya upangaji wa matumizi ya ardhi na kuhimiza uandaaji na utekelezaji wa mipango ya matumizi
ya ardhi katika miji, miji midogo na vijiji,”amesema.
Ametaja changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya ardhi nchini ikiwemo upungufu wa Wataalam wa Mipangomiji walioajiriwa na Serikali, upungufu wa vitendea kazi, ufinyu wa bajeti ili kukidhi hatua za kutwaa, kupanga, kupima na kumilikisha Ardhi.
“Ni kweli kwamba kuna changamoto ya uhaba wa Wataalam wa Mipangomiji katika Bodi yetu na nchini kwa ujumla ili kukabiliana na changamoto hii Bodi kwa kushirikiana na Wizara yangu, itaendelea kuomba vibali vya uhamisho wa watumishi kuhamia Bodi, kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na kuwajengea uwezo watumishi waliopo,”amesema.
Hata hivyo Ridhiwani amesema kuwa kuwepo kwa kampuni 81 za upangaji miji kwa namna moja au nyingine umepunguza uhaba wa watumishi kwa kufanya kazi ya kupanga maeneo katika sehemu mbalimbali nchini,kazi ambayo ingepaswa kufanywa na Wataalam wa Wizara ya Ardhi.
Hongereni sana! Aidha, pamoja na uzinduzi wa Bodi mpya nitakaoufanya leo, natambua kuwa Mwenyekiti na baadhi ya Wajumbe walioteuliwa walilitumikia Taifa kupitia Bodi kwa kipindi cha cha miaka mitatu kilichoishia mwezi Machi, 2022.
Kwaupande wake Msajili, TP.Lucas Mwaisaka amesema kuwa bodi hiyo imeundwa na wajumbe tisa ambapo bodi iliyomaliza muda wake Machi 28, 2019 ambapo imemaliza muda wake Machi 27,2022.
TP.Mwaisaka ametaja majukumu ya bodi hiyo kuwa kuimarisha maadili na utendaji kazi kwa Wataalam wa Mipangomiji kuweka utaratibu wa kusajili Wataalam Mipangomiji wenye uwezo na uzoefu kulingana na matakwa ya sheria,kusaidia kufanyamchakato wa pangaji ardhi kuwa wa uwazi na uhakika.
Kuinua kiwango cha uwezo wa wataalam wa mipangomiji kwa njia za mafunzo,kuhamasisha Wataalam wa Mipangomiji kutumia taaluma zao kufikia jamii,kutoa elimu kwa ilikuelimisha wananchi masuala ya ukuaji wa miji ilikupunguza tatizo holela la miji.
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari