*Asisitiza wananchi kupiga kura
*Asema mazingira ni rafiki na usalama upo
Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Mgombe Udiwani wa Kata ya Pasiansi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),jimboni Ilemela mkoani Mwanza,Regina Lubala (PACOME),ameungana na wananchi wa Kata hiyo katika zoezi la kupiga kura.
Ambapo leo Oktoba 29,2025, Tanzania inafanya uchaguzi mkuu wa kuchagua Rais,Wabunge na Madiwani,ambao wataongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Regina,ambaye ameungana na wananchi kupiga kura katika kituo cha Sunrise Sekondary A3,Kata ya Pasiansi.
Baada ya kupiga kura,Regina ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wananchi wa Kata ya Pasiansi na Tanzania kwa ujumla kujitokeza kupiga kura katika vituo kwani mazingira ni rafiki na hali ya usalama ni wa kutosha.




More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako