Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (MNEC),Dkt.Angeline Mabula, ameungana na wananchi wa Kata ya Kirumba na taifa kwa ujumla,kujitokeza kupiga kura la kuchagua viongozi katika nafasi ya urais,ubunge na udiwani.

Dkt.Angeline,amefika mapema leo Oktoba 29,2025,katika kituo cha kupigia kura cha Kirumba Kati C1,Kata ya Kirumba jimboni Ilemela mkoani Mwanza,akiwa miongoni mwa wapiga kura wa kwanza kushiriki katika zoezi la kupiga kura kituoni hapo.
Baada ya kutekeleza haki yake ya kidemokrasia na kikatiba,Dkt.Angeline ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la kupiga kura, akisisitiza kuwa ni fursa muhimu ya kuchagua viongozi wanaostahili kuwatumikia huku hali ya usalama ikiwa ni shwari.


More Stories
Milioni 299 kutumika kujenga ofisi za kata
Mtanda asisitiza matumizi ya takwimu serikalini
Maofisa Habari watakiwa kuhabarisha taarifa sahihi