December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC:Makala atoa agizo kwa Jeshi la Polisi Dar

Na Heri Shabani,timesmajira,online

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Amos Makala ametoa agizo kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum  Dar es Salaam kuanza oparesheni Maalum ya kuwakamata wahalifu  katika Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa Amos Makala ameyasema hayo jana jijini humo,wakati wa majumuisho ya ziara yake  ya utatuzi wa kero za wananchi katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo .

” Naagiza kwa Jeshi la Polisi Kanda  Maalum Dar es Salaam kuanzia leo muanze oparesheni ya kuwakamata waharifu wote ndani ya mkoa huu kero kubwa wananchi wetu wanakosa amani “amesema Makala.

Ameagiza hilo kushirikiana na Ulinzi Shirikishi katika oparesheni ya kamata  vibaka ambayo inatarajia kuanza Leo(jana) rasmi.

Aidha Makala amewataka wazazi wa mkoa huo kukaa na watoto wao kuwauliza kazi wanazofanya vizuri wasije wakaingia katika mikono ya Sheria kwa ajili ya uhalifu.

Amesema katika mkoa wa Dar es Salaam uhalifu umeongezeka ukiwemo wizi wa vifaa vya magari ambapo wamiliki wanapofatilia wanakuta  wanauziwa kifaa hicho hicho cha gari lake.

Katika hatua nyingine,Makala amesema katika  ziara aliyoifanya ameona kumekithiri migogoro ya ardhi kutokana na wananchi kutapeliwa na wengine kuziwa mara mbili.

Amesema  jumla ya kero zote alizopokea ni  kesi 927 kati ya kesi hizo kesi 300 za mgogoro ya ardhi amezitatua.”Nazitaka Idara ya ardhi kuongeza kasi katika utatuaji migogoro mbalimbali ya ardhi huku akigiza Halmashauri husika kuwa wawazi katika utatuzi wa kesi hizo,”amesema

Kwa upande wake Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam Jumanne Mulilo amesema amepokea agizo la mkuu wa mkoa atatekeleza .