May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC.Mrindoko: wakulima wa tumbaku wenye madai ya fedha sasa kulipwa

Na George Mwigulu, Timesmajira Online,Katavi.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewahakikishia wakulima wa zao la Tumbaku katika msimu wa kilimo 2022/2023 ambao hawaja lipwa fedha zao zaidi ya Dola milioni 2.5 kwenye AMCOS 6 zilizoingia mkataba wa ununuzi wa zao hilo kampuni ya Mkwawa Leaf LTD zinatarajiwa kulipwa hivi karibuni na kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko aliwahakikishia wakulima wa AMCOS sita ambazo hazijalipwa Fedha ya mauzo ya Tumbaku tayari serikali imefanya jitihada Kupitia Rais Dkt Samia Saluhu Hassan amefanya jitihada kubwa za kuhakikisha wakulima hao wanalipwa fedha zao hivi karibuni kuanzia tarehe 4 septemba na kuendelea wataanza kulipwa .

Amebainisha kuwa Serikali ya Mkoa wa Katavi inafahamu kuna wakulima wa Tumbaku hawajalipwa fedha zao kwa wakati walizouza Tumbaku yao kwa msimu wa mauzo ya tumbaku ya mwaka huu.

Amezitaja Amcos sita ambazo hazijalipwa fedha zao na Kampuni ya Mkwawa kuwa ni Nsimbo,Bulamata ,Magunga ,Kasekese , Muungano na Ilunde

Mrindoko alisema Jumla ya fedha ambazo wakulima wa Amcos hizo wanazodai Kampuni ya Mkwawa ni Dola za Kimarekani Milioni 2.582 tatizo la wakulima kutolipwa fedha zao kwa wakati si Mkoa wa Katavi peke yake na limetokana na matatizo ya kiuchumi duniani ulisababishwa na uhaba wa Dola .

Hivyo aliwaelekeza wakuu wa Wilaya wote wa Wilaya zilizopo katika Mkoa wa Katavi kusimamia fedha hizo mara baada ya kuwa zimeingia kwenye Akaunti za Amcos wahakikishe wakulima wanalipwa malipo yao kwa haraka pasipokuwa na kucheleshwa hata kidogo .

Mrindoko alieleza kuwa Rais Dkt Samia amefanya kazi kubwa hivyo anawahakikishia wakulima wa Mkoa wa Katavi malipo wanayodai wakulima watalipwa hivi karubuni kwani wakulima watambue kuwa Serikali ipo pamoja nao siku zote kuhakikisha haki ya kila mkulima inapatikana .

Aidha amewataka wakulima wa zao hilo kuendelea kulima kwa bidi kwani hawatarajii tena kuona tatizo hilo linaendelea tena kwenye msimu ujao wamejipanga kuondoa tatizo hilo kwa kuyasimamia kikamilifu makampuni ya ununuzi wa Tumbaku .

Katika Mkoa wa Katavi kuna makampuni mawili ambayo yanayonunua Tumbaku ambayo ni Premium ambayo imeisha lipo kiasi cha Dola milioni 19.598 na wao hawadaiwi hata senti moja na wakulima wao kampuni ya pili ni ya Mkwawa ambao wao wanadaiwa na wakulima kiasi cha Dola milioni 2.582